Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imepokea jumla ya vitabu 30,364 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 118.1 kutoka Serikali Kuu kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) lengo ikiwa ni kukamilisha uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja.
Vitabu hivyo vilivyotolewa ni vya masomo ya sayansi ikiwemo Hisabati,Bailojia,Kemia na Fizikia kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne kwa shule za serikali 32 katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Baada ya kupokelewa kwa vitabu hivyo Ofisa Elimu divisheni ya Sekondari Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mwalimu Sylvester Mlimi amewaelekeza wakuu wote wa shule za sekondari ndani ya halmashauri hiyo kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri ili vitabu vitumike kwa wanafunzi wote kuanzia Jumatatu na sio kuvitunza kwenye maboksi.
Mwl.Mlimi ameeleza kuwa divisheni hiyo meandaa timu ya kufuatilia kila shule kujionea jinsi vitabu hivyo vinavyotumika kwa wanafunzi kwa lengo la kuinua taaluma.
Mwalimu wa Taaluma shule ya sekondari Bujingwa,Mwl. Sostenes Sombi ameeleza kuwa kupitia vitabu hivyo vitawasaidia katika kujifunza.
Kwa upande wake Mwandamizi taaluma shule ya sekondari Angeline Mabula Mwalimu Zitta Chambo, amesema kuwa vitabu hivyo vitawasaidia wanafunzi kujiandaa kabla na baada ya vipindi pamoja na kuwajengea uwezo wa kujiamini juu ya masomo yao.
Pia vitasaidua kuwahamasisha watoto kupendelea kusoma masomo ya sayansi huku akitoa ombi kwa serikali kuwezesha vitabu kwa wanafunzi wanosoma masomo mengine.
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi