November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ilemela yafanikiwa kukusanya asilimia 70 ya makisio ya bajeti ya mwaka 2022/23

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Hadi kufikia Desemba mwaka 2022, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 9.4(9,433,842,484.00), kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 sawa na asilimia 70 ya makisio ya bajeti ya mwaka huo wa fedha ambayo ni mapato ya ndani.

Huku kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha kiasi cha zaidi ya bilioni 1.14(1,146,470,929.84),zimeelekezwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo katika Kata zilizopo ndani ya Halmashauri hiyo.

Akisoma taarifa yake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary,katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya pili(Oktoba-Desemba) ya mwaka wa fedha wa 2022/23 kilichofanyika Februari 27, mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri.

Ambapo ameeleza kuwa kati ya fedha hizo mapato halisi ni bilioni 4.6(4,623,383,233) sawa na asilimia 35.6 ya bajeti.

Huku mapato fungwa ni milioni 151.349,995 pamoja na kiasi cha bilioni 4.6(4,659,109,256),ni mapato yalioyokana na mauzo ya viwanja.

Aidha ameeleza kuwa zaidi ya bilioni 1.14 katika robo ya pili ya mwaka wa fedha zimeelekezwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika Kata, ikiwemo sekta ya elimu, afya,utawala,biashara,uwekezaji na viwanda, miundombinu, maendeleo ya miji na vijiji,mipango miji na maendeleo ya jamii.

Mipango Miji

Ameeleza kuwa katika mradi wa upimaji wa viwanja vya Nyafula,idadi halisi ya viwanja vikivyopimwa ni 3,255 katinya hivyo viwanja 3,065 tayari vimeuzwa na jumla ya bilioni 4.6(4,659,109,256) imekusanywa huku viwanja vilivyobaki ni 190, fedha zinazodaiwa ni bilioni 7.8(7,811,375,414.06

Sekta ya Elimu

Mhandisi Modest, ameeleza kuwa kiasi cha milioni 12.5,zimetumika kwa ajili ya ukamilishaji wa darasa na ofisi moja ya Mwalimu shule ya msingi Kiseke,milioni 4.5(4,523,650), kwa ajili ya malipo ya pango la ardhi kwenye eneo lililotolewa na kanisa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Kata ya Nyasaka.

Kiasi cha milioni 10,kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Ibungilo,ujenzi wa bweni kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Buswelu ambapo kiasi cha milioni 3.1(3,190,000), milioni 2 Kwa ajili ya ununuzi wa eneo la ujenzi wa shule ya msingi Kata ya Kahama.

Milioni 15, kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Kangaye Kata ya Nyakato pamoja na milioni 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa katika shule iliopo Kata ya Kahama hivyo kufanya jumla ya ya kiasi cha milioni 97.2(97,213,650).

Sekta ya Afya
Ameeleza kuwa kiasi cha milioni 85 ujenzi wa wodi ya mama na mtoto kituo cha Afya Buzuruga,milioni 17.0(17,068,115.5), ujenzi katika hospitali ya Wilaya, matengenezo katika chumba cha X-Ray kituo cha Afya Karume mililioni 3,939,057.44.

Pia ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba za watumishi kituo cha Afya Sangabuye milioni 2.8(2,885,500), milioni 25, ujenzi wa jengo la kujifungulia wajawazito zahanati ya Nyamwilolelwa,kuweka mtandao wa maji katika kituo cha magonjwa ya mlipuko.Buswele kiasi cha milioni 3.4(3,487,648) hivyo kufanya jumla ya milioni 137.3(137,380,320.94) katika sekta hiyo ya afya.

Maendeleo ya Jamii

Mhandisi Modest,ameeleza kuwa jumla ya milioni 285,ilipekekwa kwenye vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa vikundi 37 kati ya hivyo vikundi 28 vya wanawake ambavyo vilipokea kiasi cha milioni 228.

Vijana vikundi 7 vilivyopokea kiasi cha milioni 53 na vikundi viwili vya watu wenye ulemavu vilivyopokea kiasi cha milioni 4.

“Katika makusanyi yanayotokana na marejesho ya vikundi tumefanikiwa kununua bajaji 1 ambayo amekabidhiwa mtu mwenye ulemavu wa Kata ya Pansiansi,” ameeleza Mhandisi Modest.

Miundombinu, maendeleo ya miji na vijiji

Ameeleza kuwa katika kipindi hicho cha robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2022/23 wamefanikiwa kufungua barabara ya mradi wa viwanja vya Nyafula zenye urefu wa Km 59 kwa thamani ya milioni 56.4(56,459,207) pamoja na kupasua mawe katika barabara ya Kazamoyo milioni 3.5.

Kwa upande wao baadhi ya Madiwani kutoka Kata za Halmashauri hiyo akiwemo Diwani wa Kata ya Pasiansi Rosemary Mayunga ameshauri kuwa wakati wanapotekeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa uende sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo.

“Kwasababu tunakuwa na madarasa mengi na watoto wanafaulu wengi unakuta labda wanafunzi 2000 matundu ya vyoo hayatoshelezi,”.

Baadhi ya Madiwani waliohudhuria mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kipindi robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/23 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo Februari 27,2023.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary, akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kipindi robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/23 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo Februari 27,2023.