Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
TIMU ya Ihefu FC ya jijini Mbeya imefanikiwa kupanda rasmi Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) msimu ujao na kuwashusha Mbao FC katika mchezo uliochezwa leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Ihefi inakuwa timu ya Tatu yaLigi Daraja la Kwanza (FDL) kupanda Ligi Kuu msiku ujao ikiungana na Gwamina FC ya Misungwi, Mwanza pamoja na Dodoma Jiji FC ambazo zilikuwa vinara wa kundi A na B.
Matokeo hayo pia yanaifanya Mbao kuwa timu ya tano iliyokuwa Ligi Kuu kushuka daraja na kuungana na Lipuli ya Iringa, Alliance nayo ya Mwanza, Singida United ya Singida na Ndanda FC ya Mtwara.
Katika mchezo huo wa marudiano wa hatua ya mtoano ‘Play Off’ wenyeji Mbao walipata ushindi wa goli 4-2 huku matokeo ya jumla yakiwa ni goli 4-4 na matokeo hayo kuwabeba zaidi Ihefi kwa faida ya goli za ugenini baada ya kushinda goli 2-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Highland Estate.
Mbao FC walikuwa wa kwanza kupata goli katika mchezo huo lililofungwa na mshabuliaji Waziri Junior dakika ya nane na 45, Michael Masinda aliyejifunga dakika ya 47 na goli la nne lilifungwa na Datus Peter kwa penalti dakika ya 90 wakati magoli ya Ihefu yamefungwa na Willy Mgaya na Geoffrey Kinyozi.
Katika uwanja wa Sokoine, wenyeji Mbeya City wamefanikiwa kutetea nafasi yao na kusalia Ligi Kuu Baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi yya Geita Gold.
Goli pekee katika mchezo huo lilipatikana kwa mchezaji wa Geita, Geoffrey Manyasi kujifunga kipindi cha kwanza na lililofanya Mbeya City kucheza kwa kujilinda zaidi hadi dakika 90 zinamalizika bila kuruhusu goli.
Mbeya City imebaki Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa goli 2-1 baada kupata sare ya goli 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa sekondari ya Nayankungu, Geita
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship