December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

IGP Wambura afanya mabadiliko ya makamanda

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko mbalimbali kwa baadhi ya makamanda Polisi mikoa.

Mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Oktoba 20, 2022 na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, IGP Wambura amewahamisha kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi SACP Henry Mwaibambe ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.Pia aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Safia Shomary amehamishiwa Mkoa wa Geita kuwa Kamanda wa Polisi Mkoani humo.

Aidha aliyekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Temeke jijini Dar es Salaam , Kamishna Msaidizi wa polisi ACP Richard Ngole amehamishiwa makao makuu ya Polisi Dodoma.Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Kungu Malulu ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji.