January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Idris amshukuru Rais Kikwete kwa kumpongeza kuingia Netflix

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa vichekesho hapa nchini Idris Sultan, amemshukuru Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumpongeza kuingia Netflix jambo ambalo linawapa hamasa kubwa vijana.

Akitoa shukrani hizo Kupitia katika Ukurasa wake wa Instagram yake Idris amesema, mapenzi aliyokuwa nayo Rais Kikwete kwa maendeleo ya vijana wa Kitanzania vinawapa faraja kuba sana na kujipa moyo ili waweze kufika mbali.

“Baba baba baba Jakaya Kikwete. Mapenzi yako kwangu na kwa maendeleo ya vijana wa kitanzania kama mimi ni tosha kuonesha weupe na nuru ya nafsi yako na moyo. Mwenyezi Mungu akupe mema utakayo kabla hata ya wewe kumuomba na apokee dua zetu kwako na familia yako. Nitakuwa naipost hii kila nikipata wasaa pia. Itabidi tuvumiliane humu(Mambo yameumana),” ameandika Idris

Hii imekuja baada ya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuandika ujumbe huu kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram

“Nimepata wasaa wa kutazama ‘SlayOnNetflix’ na kumuona Idris Sultan katika sinema hii. Nimefarijika sana na hatua hii aliyopiga. Ametuweka Watanzania ‘use’ wa Netflix. Ni mwanzo mzuri sana. Tumuunge mkono afanye vizuri zaidi, na azidi kututoa kimasomaso huko mbeleni,” ameandika Rais Kikwete.