Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
Idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliopo Kata ya Mchafukoge,wilayani Ilala Mkoa wa Dar-es-Salaam,imeongezeka kutoka wagonjwa 64,953 mwaka 2020 mpaka kufikia 143,803 mwaka 2024.
Mganga wa hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt.Delila Moshi,amebainisha hayo wakati Kamati ya Siasa Kata ya Mchafukoge,ikiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mariam Lulida,ilipofanya ziara katika hospitali hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Mbali na hospitali ya kisasa ya Mnazi Mmoja iliyojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wa KOICA ,pia ilitembelea shule ya sekondari Jamhuri,mradi wa Mwendokasi Kasi na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini( LATRA .)
Dkt.Moshi ,amesema hospitali hiyo ina watumishi 196 wa kada mbalimbali,licha ya idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa kuongezeka pia wateja wa Kliniki ya Baba ,Mama na Mtoto na vijana imeongezeka na kufikia 20,166 mwaka 2024.
Huku idadi ya wajawazito wanaopatiwa huduma katika hospitali hiyo imeendelea kuongezeka kutoka wajawazito 3,706 mwaka 2020 hadi 3,854 mwaka 2024.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mchafukoge Mariam Lulida,kamati ya Siasa ya Kata hiyo ,imejiridhisha na kazi uliofanywa na Serikali,kwani wamejionea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri, Serikali Kuu na ya kimkakati.
“Hospitali ya Mnazi mMmoja ni miongoni mwa vituo vya kutolea huduma za afya za Serikali kilichopo Kata ya Mchafukoge,tumepata mafanikio katika hospitali hiyi ikiwemo upanuzi wa jengo kwa mapato ya ndani ,kuanza kwa mchakato wa kuanzisha wodi ya watoto wanaozaliwa na changamoto (NICU),ambapo tumepata milioni 25 kutoka kwa wadau ,kuanzisha kwa mchakato wa ujenzi wa hospitali ya kisasa,”.
Akizungumzia sekta ya elimu Lulida,amesema shule ya sekondari Jamhuri, ni shule kongwe ambapo milioni 200 zimetumika kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya yake,inayoongozwa na wazazi na uongozi wa shule.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kata ya Mchafukoge, Jammal Abubakar,amesema wameridhishwa na utekelezaji wa Ilani iliofanywa na Diwani Mariam Lulida huku akiwataka WanaCCM kutembea kifua mbele.
More Stories
EWURA yatangaza bei kikomo za mafuta
Fainali Khimji cup kufanyika Februari 7,2025
Dkt.Serera apongeza utendaji kazi wa Wakala wa Vipimo