September 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Huduma Mhakama ya Mwanzo Uyole zarejea

Na Esther Macha,TimesMajira Online. Mbeya

HATIMAYE huduma za kimahakama zilizokuwa zimesimama katika Mahakama ya Mwanzo, iliyopo eneo la Uyole jijini Mbeya baada ya jengo lake kuteketea kwa moto mwaka 2018, zimerejea rasmi baada kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya.

Mahakamna hiyo ilichomwa moto mwaka 2018 na watu wasiojulikana, waliokuwa wanakabiliwa na mashauri katika mahakama hiyo.

Hayo yamesemwa jana na Ofisa Utumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Rajab Singana wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo jipya katika uzinduzi wa jengo hilo jipya.

Singana amesema kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, inadhaniwa wananchi wasiojulikana waluiokuwa wanakabiliwa na mashauri katika mahakama hiyo, ndiyo waliohujumu miundombinu ya ofisi hiyo kwa kile kilichodhaniwa kuwa kutoridhika na mienendo ya uendeshaji wa mashauri katika mahakama hiyo.

Amesema moto huo ulisababisha hasara kubwa zikiwemno kuungua samani zote za ofisi, majalada na vielelezo vya mashauri vilivyokuwa vimehifadhiwa ndani ya jengo hilo, ambapo kulikuwa na jumla ya majalada ya mashauri 656 ambayo yaliteketea kwa moto na kuifanya mahakama kushindwa kuendelea na mashauri hayo.