Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya imepokea mashine mbili za kusaidia mfumo wa upumuaji na kuzalisha hewa safi(oxygen)kutoka Shirika la Gradian Health System zenye thamani ya shingi milioni sabini ili uimarisha kitengo cha wagonjwa mahututi(ICU).
Akikabidhi mashine hizo za kisasa leo msemaji wa Shirika la Gradian Health System, Ibrahim Bakari amesema mahusiano mazuri na hospitali hiyo ndicho kilichowasukuma kutoa mashine hizo na kuahidi kujenga maabara ya vifaa tiba ili kuwafundisha madaktari na watumiaji wa vifaa tiba.
Bakari amepongeza Uongozi wa hospitali kwa kuendelea kuboresha huduma na kusema kuwa msaada huo wa vifaa tiba ni matokeo mazuri ya mahusiano yaliojengeka kati ya hospitali na taasisi ya Gradian Health Systems hivyo anaimani kuwa vifaa tiba hivyo vitatumika vizuri katika kuwahudumia wananchi na kuahidi kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya sita katika maboresho ya huduma za afya nchini.
Akipokea vifaa hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt.France Rutwashoba amelishukuru Shirika la Gradian Health Systems kwa msaada wa mashine mbili za kuwasaidia wagojwa walio mahutiuti kupumua zenye thamani ya shilingi milioni 70 kwa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.
Dkt. Rutwashoba amesema kuwa mashine hizo ni kwaajili ya wodi ya wagonjwa mahutihuti (ICU) lengo likiwa ni kuendelea kuiunga mkono Serikali ya maboresho ya sekta ya afya nchini
Akizunguza wakati wa makabidhiano ya mashine hizo Dkt. Rutwashobaamesema kuwa mashine hizo zimekuja kwa wakati muafaka na kuwa ni za teknolojia ya kisasa pia ni rafiki kwa watumiaji hivyo zitaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa watumishi kuzitunza vizuri pamoja na kutumia muda mwingi kuendelea kujifunza namna inavyo fanya kazi kutokana na usasa wa mashine hizo kuwa za teknolojia mpya.
Dkt. Amos Zacharia ni Mtaalamu wa utoaji salama wa dawa za usingizi na ganzi ameushukuru Uongozi wa Hospitali pamoja na wadau Gradian Health System kwa ushirikiano katika kuhakikisha jamii inapata huduma bora za afya kwa kuboresha miundo mbinu.
Aidha Dkt Zacharia amesema kuwa vifaa tiba hivyo vitatumika vizuri katika kuongeza ufanisi wa utoaji huduma katika idara ya magonjwa ya dharura na ajali, wodi ya wagonjwa mahutihuti na wagonjwa waliotoka katika upasuaji.
Shirika la Gradian Health Systems ni moja wa wadau wakubwa wa maendeleo katika sekta ya afya nchini wanaojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa vifaa tiba katika eneo ya lada za usingizi na mashine za kusaidia kupumua wagonjwa mahutiuti “ventilators”.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa