November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya yapokea msaada wa vifaa tiba

Na Esther Macha,Timesmajira,Onlline, Mbeya

HOSPITALI ya Rufaa Kanda ya Mbeya imepokea msaada wa vifaa tiba kutoka Benki ya Maendeleo ( TIB )kwa ajili kuokoa maisha ya watoto njiti kitengo cha wazazi Meta kwa ajili ya kuwahudumia watoto hao .

Imeleezwa kuwa msaada huo wa vifaa tiba utaweza kusaidia kuendelea kutoa huduma kwa watoto njiti katika hospitali ya wazazi Meta kitengo cha watoto njiti ambao wanazaliwa kabla ya muda.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo Daktari Bingwa wa watoto Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, Dkt. Angela Leonard amesema kuwa vifaa tiba hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa ajili ya kusaidia watoto wachanga kwa ajili ya kuokoa maisha yao.

“Kikubwa tunaendelea kutoa wito kwa sekta zingine kuendelea kujitokeza kusaidia watoto wachanga njiti kwani tuna mahitaji mengi kwa watoto hao ili tuweze kuokoa maisha ya yao ,tunashukuru sana benki hii kwa kutusaidia kitengo hiki kwa vifaa tiba hivi,”amesema Dkt. Leonard.

Meneja wa TIB Mbeya Bryason Mwanga amesema kuwa kama benki ya maendeleo kazi yake kubwa ni kutoa mikopo kwenye sekta zote za kiuchumi pamoja na huduma mbali mbali ikiwemo huduma za afya.

“Tumerejesha kwa jamii kile kidogo tulichopata, ikumbukwe kuwa hii ni siku maalum kwetu kufanya jambo letu kama jitihada zetu za kuunga mkono serikali katika kuboresha shughuli za kijamii hasa upande wa afya tukigundua kwamba kuwa kitu kikubwa katika maendeleo ya taifa lolote ni afya ya watu wake hivyo tukaona tuanze na watoto ambao wamezaliwa muda wao haujatimia”amesema Meneja huyo.