December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hospitali ya MIRACOLO kutoa huduma za Afya bure

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, (Ilala)

HOSPITAL ya MIRACOLO ikishirikiana na tawi lao jipya MIRACOLO SPECIALIZED POLYCLINIC lililopo Tabata-Kimanga inatarajia kutoa huduma za Afya Bure siku ya Julai 22 mpaka Julai 24 mwaka huu 2022.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam Mkurugenzi wa Hospitali za MIRACOLO Dkt.Anna -Pendo Deogratias alisema matibabu hayo yatatolewa kwa siku tatu ni upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Homa ya INI kisukari pressure na kutoa chanjo ya Homa ya INI Bure kabisa,hivyo amewataka Wananchi kujitokeza kupima Afya zao .

“Hospitali yetu ya MIRACOLO iliyopo Segerea imefungua Tawi jipya MIRACOLO SPECIALIZED POLYCLINIC lililopo Tabata Kimanga,Njia panda kwa Doni.

Dkt.Anna alisema hospitali ya MIRACOLO Ina madaktari Bingwa wa magonjwa mbali mbali ikiwemo Madaktari wa magonjwa ya Wanawake Watoto,Daktari wa upasuaji, Daktari wa Koo na Pua na huduma za Kinywa na Meno, na Maabara ya kisasa .

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kupima Afya zao siku hiyo kwani MIRACOLO Hospitali inajali Afya za Wananchi wakati wote ndio maana wametoa hofa hiyo katika kupima Afya zao .