Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Kyela
MKUU wa mkoa wa Mbeya,Juma Homera ameziagiza halmashauri zote mkoani humo kutoa elimu kwa Madiwani kuhusiana na mfumo mpya wa ukusanyaji mapato (Tausi) ili kudhibiti upotevu wa mapato wa halmashauri husika.
Amesema kuwa elimu hiyo itasaidia Madiwani kuona umuhimu na raha ya kukusanya mapato pamoja na kuyatumia na kuthibiti upotevu wa fedha.
Homera amesema hayo Juni 13,2023 wakati akifunga hoja za Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali wilayani Kyela mkoani hapa ambapo katika mkutano huo umehusisha madiwani, wakuu wa idara na watumishi wa halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama.
Homera ameeleza kuwa halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya zinatakiwa kuelimisha madiwani kuhusu mfumo huo wa ukusanyaji mapato wa tausi wajue faida zake na umuhimu wake na namna ya kushirikiana na wakuu wa idara katika ukusanyaji mapato.
“Huu mfumo wa tausi ndo umeletwa kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya,sasa Ofisa Mapato na uongozi wa halmashauri hii hebu tengenezeni semina maalum kwa madiwani hata ya siku moja ya kuwaelimisha ili wakasaidie ukusanyaji mapato,”amesema.
Ameongeza kuwa “ Hii treni ya wote haichagui vyama vya siasa hakuna kuachana hapa hii treni ya Mama Samia Suluhu Hassan tusiachane nje mtu akadondoka tukamwacha,wote waone raha ya kukusanya mapato siyo kuuliza mtendaji umepeleka hela,”.
Aidha Homera amezungumzia suala la ukusanyaji mapato kwa wilaya hiyo amesema kuwa imefanya vizuri kwani ilitakiwa kukusanya zaidi ya bilioni 4,mpaka Juni 9, 2023,lakini imeweza kukusanya zaidi ya bilioni 4 sawa na asilimia 99.
“Ndugu zangu wanakyela naomba muache tabia ya kuiua Kyela kimapato naomba ziishe, Madiwani kuna wengine hawaitakii mema Kyela kabisa tusiwadanganye wananchi si mmeona ufuta kule Songwe wameuza 3700 wakati uuzaji holela ulikuwa shilingi 500 tuache kudanganya na serikali imeshatoa maelekezo mazao ambayo yapo kwenye stakabadhi ghalani kupitia ushirika inaeleweka “amesema.
Diwani Vitimaalum Kata ya Dandalo wilayani Kyela , Tumaini Mwakatika amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni tanuri ambalo linapika vizuri viongozi ambao wanafanya kazi vizuri kwa weledi mkubwa uliotukuka.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango