Na Aveline Kitomary,TimesMajira Online,Dar es Salaam
TATIZO la kupoteza kumbukumbu linaathiri watu milioni 50 kote ulimwenguni ripoti hii ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo idadi ikitarajiwa kuongezeka mara tatu ifikapo mwaka 2050.
WHO inasema gharama za malezi ya watu walipoteza kumbukumbu ni kubwa inakadiriwa ifikapo mwaka 2030 itafikia dola trilioni 2 kila mwaka.
Watu wenye ugonjwa huo wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo unyanyapaa kutokana na ukosefu wa taarifa .
Kwani tatizo la kupoteza kumbukumbu inasababisha mtu kupoteza uwezo wa kuelewa, unaathiri kumbukumbu, mawazo na uwezo wa kujifunza.
KUMBUKUMBU NI NINI
Hii ni hali ya kuweza kutambua jambo uliloliona au kuweza kufafanua, kueleza jambo ulilolihifadhi ndani ya kichwa kwa muda mfupi au mrefu.
Katika Jarida la Afya leo tunaangazia sababu za kupoteza kumbukumbu kwa wazee huku wengine wakiwa hawapotezi kumbukumbu.
Daktari Bingwa wa Ubongo Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu Kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Laurent Lemery Mchome anasema kuwa watu wenye umri wa utu uzima wanahatari ya kupoteza uwezo wa kumbukumbu kutokana na sababu mbalimbali.
“Umri wa uzee tunaoongelea hapa ni kuanzia miaka 65 na kuendelea, tunaongelea kuwa watu katika kundi hili wanakuwa na matatizo ya kumbukumbu wanaweza kuwa wanasahau lakini pia kati ya kundi hili kuna ambao hawapotezi kumbukumbu kiasi na wengine sana wengine wakifikia miaka 90 hadi 100 kumbukumbu hazipo kabisa ni kitu gani kinatokea.
“Katika u b o n g o w a binadamu na hata mnyama kuna sehemu maalum z a k u t u n z a kumbukumbu na katika mchakato wa kutunza zinapitia madaraja mbalimbali wakati zinaenda kutuzwa ili ziwe za muda mrefu zinazokumbukika kirahisi bila kufikiri kwa muda mrefu.
Anaendelea kueleza “Katika mchakato huu zinaanza kwanza kupimwa kama za muda mrefu lakini baadae zinatengenezwa zinakuwa za muda mrefu hata ukiamka ukaambiwa nne mara nne unajua kuwa ni 16 japo ulijifunza ukiwa darasa na la tatu na hujaendelea kujifunza lakini unakumbukumbu kwa sababu ulirudia mara nyingi Hili ndilo kundi lililo hatarini kupoteza kumbukumbu kwa hiyo kuna sehemu za ubongo zina kazi hii.
D k t . M c h o m e a n a s e m a mara nyingi hizo sehemu ndio zinazoathirika panapotokea matatizo au umri unapokwenda.
KINACHOTOKEA UZEENI
Kwa mujibu wa Dkt.Mchome mtu anapofikia umri wa miaka 60 hadi 65 mzungunko wa damu unaanza kubadilika ile mishipa midogo sana inayokwenda sehemu za ndania za ubongo inaanza kupoteza utendaji kazi wake.
Anasema hatua hiyo inafanya damu kufika kidogo hasa pale mtu anapokuwa hajishughulishi na kazi au ufanyaji mazoezi.
“Na kama mtu anakuwa amekaa tu kwa sababu ya uzee na ugonjwa damu inakuwa haizunguki vizuri sana kama mtu anayetembea na kufanya mazoezi ufikaji wa damu katika lile eneo unakuwa kidogo na matokeo yake kumbukumbu zinaathirika anaanza kusahau lakini miaka vinavyokwenda anasahau zaidi na zaidi.
“Pia kuna magonjwa maalum kama magonjwa ya mtikisiko wa ubongo na kufa kwa seli za ubongo (alzheimers na Dimetion) haya yanaathiri kumbukumbu kwa kiasi kikubwa,unathiri zile sehemu kwa kiasi kikubwa na watu hawa wanapoteza kumbukumbu wanakuwa kama watoto wadogo hawakumbuki umri unavyozidi kwenda hata watoto wake wa kuwazaa hakumbuki hata mmoja .
“Kwa hiyo damu inavyokwenda kupeleka oksijeni na chakula sehemu za mwili na ubongo zilizo ndani kabisa ile mishipa midogo inapoteza nguvu za kupeleka damu taratibu kumbukumbu zinapungua kwa sababu lile eneo linashindwa kufanya kazi kama ujanani zile chembe hai hazipati chakula cha kutosha baadae ya mishipa kupungua nguvu, yapo magonjwa mengi hata zaidi 50 yanaathiri uwekaji wa kumbukumbu,” anaeleza Dkt.Mchome.
Anasema magonjwa hayo ya kumbukumbu yanaweza kuambatana na magonjwa kama kutembea kwa shida, kuona, tatizo la kushindwa kuzuia mkojo na matatizo mengi.
AMBAO HAWAPOTEZI KUMBUKUMBU
Dkt.Mchome anabainisha kuwa kuna watu wana miaka 85 hadi 90 na bado wanakumbukumbu vizuri hii inatokana na utofauti wa miili ya binadamu kulingana na aina ya maisha waliyokuwa wakiishi kipindi cha nyuma.
“Wapo watu wana miaka mingi na wanakumbukumbu lakini utakuta mwenzake ana miaka 70 kumbukumbu zimekwisha miili ya binadamu tunatofautiana sana na jinsi tulivyoumbwa kuna mwingine tatizo linaanza mapema na mwingine asipate kinachoamua sana ni aina ya maisha.
“Mfano kushughulisha mwili kama kijijini watu wanashughulisha miili na hapa mjini kuna watu wanafanya mazoezi na kufanya mwili kuwa active hivyo maisha ya mtu yasipohusisha mazoezi ni hatari kwa utunzaji wa kumbukumbu,” anadadavua.
LISHE INACHANGIA
Mtaalamu wa lishe kutoka taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Adeline Munuo anasema nafasi ya vyakula katika utunzaji wa kumbukumbu ni muhimu zaidi kutoka na vyakula kuwa na uwezo wa kusaidia ubongo.
Anasema ulaji wa vyakula mchanganyiko ni muhimu zaidi ili kila sehemu ya mwili kupata kirutubishi kinachohitajika.
“Vipo vyakula ambavyo vinasaidia kuimairisha afya ya ubongo kama mafuta ya samaki yanaimarisha afya ya ubongo na mishipa ya fahamu,mafuta ya sangara na sato yanafaa zaidi ni muhimu inawezesha kutunza kumbukumbu katika ubongo na seli za ubongo hazitapata shida.
“Kuna tafiti mbalimbali ya mwaka 2017 inaonesha watu wenye mafuta ya Omega3 wamekuwa na kumbukumbu nzuri kutokana na ubongo kuwa na mtiririko mzuri wa damu wana uwezo wa kufikiri.
“Vyakula vingine ni dagaa, binzari au manjano ina kiambata inyoboresha ubongo kwa kuboresha seli za ubongo na kupunguza msongo wa mawazo na uwezo wa kukumbuka.
“Chakula kingine ni brokoli ni mbogo aambayo inavitamini K na C ambayo inaimarisha kinga ya mwili inasaidia na magonjwa ya uzee kama kupoteza kumbukumbu na pia inaondoa sumu, ubongo unapokuwa umepata msongo inatengeza sumu lakini ukitumia brokoli inasaidia kuondoa sumu mwilini,” anafafanua.
Anabinisha vyakula vingine kuwa chai ya kijani (green tea) ambayo inacafen inayosaidi kujisikia utulivu na ubongo kuwa na upumzika na mbegu za mabogo ambazo zina kiwango kikubwa cha Zinc inayosaidia kuongeza kumbukumbu.
“Lakini mbegu hizo zina vitamin E, ina kiasi cha mafuta cha Omega 3 ambayo inamasaiada kwa ubongo unaweza kukaanga na kutumia kwa kutafuna kama karanga.
“Kitu kingine ni nyanya ni muhimu kwa kuzuia mgonjwa ya ubongo inasaidia ubongo kupata kinga dhidi ya mgonjwa na unaimarisha afya ya ubongo, karanga zina mafuta mazuri kwa ajili ya mafuta ya Omega3, zina vitam D inayoweza kulinda seli na stress tofauti tofauti utafiti wa mwaka 2014 unasema kuwa na vitamin E inasaidia kukumbuka na kupunguza magonjwa ya uzeeni,” anaeleza.
Anasema zingine ni mbegu za alizeti, ufuta, mayai, nafaka zisizokobolewa zinazuiaa mgonjwa mengi ikiwemo magonjwa ya ubongo na mfumo wa fahamu, mafuta ya parachichi ambayo pia hupunguza shikizo la damu ina mafuta mazuri kwa afya ya ubongo.
“Ni muhimu kuchanganya milo yetu tena zenye rangi tofauti tofauti ili kuweza kusaidia mwili kwa sababu uwezekano wa mtu kupoteza kumbukumbu inakuwa sio rahisi vyakula hivyo viliwe kwa mchanganyiko.
ATHARI ZA KISAIKOLOJIA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge, Christian Bwaya anasema zipo mbinu za kisaikolojia ambazo zinweza kufanya mtu kutopoteza kumbukumbu.
Msaikolojia huyo utunzaji wa kumbukumbu linaweza kuwa la athiri kutoka kizazi hadi kizazi.
“Kuna watu wanazaliwa wakiwa na uwezo wa juu wa kumbukumbu, kuna kumbukumbu za aina tatu mfano kufumba macho na kufumbua, kuna kumbukumbu ya muda mfupi na kumbukumbu ya muda mrefu ambao hautasahu.
Anaainisha za kutunza kumbukumbu ikiwa ni pamoja na umakini, tabia ya kujielekeza katika kitu kimoja ambazo utakumbuka kwa muda mrefu na hautasahau.
“Mbinu ya pili kwenye kumbukumbu ya muda mfupi kama namba ya simu hizo namba unakumbuka baada ya kurudia rudia inakaa kichwani, kwa hiyo kama unataka uweke vitu kichwani rudia rudia watafiti wanasema kama nitahusisha hicho kitu sitasahau na kile ambacho unacho.
“Mbinu nyingine ni ya kupangilia vitu kila kitu kikae mahali pake ukiwa mtu wa kupangilia inakuwa si mtu wa kusahau unakariri maeneo,” anasema.
Anabainisha kuwa sababu za watu wazima kushindwa kuwa na kumbukumbu kisaikolojia ni kushindwa kuzingatia kitu kimoja.
“Kingine anaweza kuwa anapuuza vitu hii inazuia kuhifadhi vitu kukosa ‘interest’ anapokutana na taarifa mpya, mzee tayari ana mambo mengi na yanaingiliana kwa hiyo inakuwa inaingiliana asipokuwa makini.
“Utakuta ana vitu vingi kichwani na vinachanganyikana na apotaka kutafuta hapati, ni lazima aingize kumbukumbu kwa milango ya fahamu na kwa sababu mwili umechoka hawezi kuingiza kumbukumbu kirahisi,” anaeleza Bwaya.
NJIA YA KUMSAIDIA
Mtaalmu wa mazoezi kwa njia ya vitendo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt.Marion anasema wanawasaidia wagonjwa hao ili kupunguza athari za upotevu wa kumbukumbu.
“Tunaweka utaratibu wa kila siku mfano mgonjwa atakapoamka ataanza kupinga mswaki kitendo kitajirudiarudi ili awe na kumbukumbu.
“ Tu n a m s a i d i a k u m u d u kumbukumbu tuna daftari la kumbuku ambalo litaonesha kitendo na muda unaotakiwa, tunatumia picha za familia ambazo zina sura na majina wapo wanaoona picha akakumbukua lakini jina hakumbuka na pia anaweza kukumbuka jina na picha hakumbuki.
Anasemaa wanatumia picha za vitendo ili aweze kuelewa kitendo ambacho anatakiwa kufanya kwa wakati ule.
“Mfano kula unamwekea mtu anayekula unamwambia kula halafu anakula,wengine wanashida ya kufuatilia dawa unaweka picha ya dawa anakuwa anakumbuka.
“Kwa mgonjwa anaweza kulindwa kuwe na mtu maalum kuwe na geti na akitoka afuatiliwe kwa ukaribu kama mfano nyumbani anapikia gesi tunamwekea karatasi ya kumkumbusha iliyoandikwa ‘zima gesi’.
IDADI YA WANAOUGUA
Dkt.Marion anasema kwa watu wazima au wazee wanaweza kuona wagonjwa wanne wapya kwa kila wiki.
“Tunawafuatilia hapa nyuma historia yao ilikuwaje na kama wakiugua na kupoteza kumbukumbu tunawafundisha maneno ili kusaidia kurudisha kumbukumbu.
“Kuandika maneno kila siku na kurudia rudia mpaka aweze kukariri, kurudia rudia vitu mbalimbali ili Hili ndilo kundi lililo hatarini kupoteza kumbukumbu kuweza kurudisha kumbukumbu.
MAZOEZI NI MUHIMU
Dkt. Mchome anashauri kuwa mazoezi ni muhimu kusaidia kuepukana na tatizo la kumbukumbu.
“Ni muhimu kutengeneza mfumo wa mazoezi kwa kila wiki mara moja au mbili na inategea aina ya mazeozi na pia ni muhimu wakapata ushauri wa mtaalamu wa afya ili waweze kujua aina ya mazoezi kulingana na jinsi walivyo kama wana magonjwa mengine .
“Lakini pia kuna ‘sapliment’ ambazo zinasaidia mfumo wa fahamu kuwa katika hali nzuri na kukumbuka vitu vingine zinakuwa ‘sapliment’ za kawaida kwa ajili ya kuzuia upotevu wa kumbukumbu.
“Na pia kwenda hospitali kufanya uchunguzi wa afya yako kwa vitu vyote kama damu,moyo ,figo na mengine hata kama huumwili chunguza afya. Kwa upande wa anawashauri kufanya mazoezi ili kuwasaidia watakapolekea kipindi cha uzee.
“Na pia kuna faida nyingi ikiwemo kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama moyo, kisukari na mengine.
More Stories
Madaktari bingwa wa Samia watua Rukwa
Utashi wa Rais Samia na matokeo ya kujivunia vita dawa za kulevya nchini
Uwekezaji wa Rais Samia sekta ya afya waendelea kuwa lulu Afrika