January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hawa hapa washindi wa ‘Wakishua Twenzetu Qatar na Hisense ‘ wiki ya tano

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

SASA ZIMEBAKIA WIKI MBILI , TIKETI 15 NA vifurushi vya vifaa vya nyumbani 20 kutoka Hisense kutolewa.

Kampuni inayoongoza Tanzania katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidijitali Tigo Tanzania, kupitia Promosheni yake ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense kwa kushirikiana na kampuni ya HISENSE wameendelea kutoa tiketi za kwenda Qatar kushuhudia kombe la Dunia na zawadi ya Vyombo vya ndani kama vile Friji , Spika za Mziki (SubWoofer), Smart Tv , pamoja na Microwave , na sasa zimebaki wiki mbili za promosheni hii na Jumla ya washindi 15 wa tiketi na 20 wa Vifaa vya Hisense wanahitajika ndani ya wiki hizi mbili.

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema kuwa” Hawa washindi wa leo wamepatikana kwenye Droo yetu ya wiki ya tano ya promosheni yetu , walifanya miamala kama kulipa bili , kufanya malipo ya kiserikali , kupokea pesa kutoka nchi za nje , benki , mitandao mingine , LIPA KWA SIMU , kununua muda wa maongezi , kuchukua mikopo ya Tigo Pesa na huduma nyingine mbalimbali za Tigo Pesa ambapo baada ya kufanya ivyo waliingia kwenye droo na mwisho wa siku kuibuka washindi wa Kampeni hii Ya WAKISHUA TWENZETU QATAR NA HISENSE ,

” Tunawasihi wateja wetu endeleeni kufanya miamala na Tigo Pesa ili kuibuka mshindi , na sasa zimebaki wiki mbili na ndani ya wiki hizihizi mbili tunawatafuta washindi 15 watakaokwenda kushuhudia kombe la dunia mubashara na washindi washindi 20 watakaojipatia kifurushi cha vifaa vya ndani vya Hisense.nawasihi mfanye miamala mingi na kutumia huduma za Tigo Pesa ili kuibuka mshindi wa zawadi hizi zilizobaki .”

“Kumbuka wale washindi wetu wa Safari ya kwenda kushuhudia kombe la Dunia Qatar , safari yenu iliyolipiwa kila kitu itaanzia Airport Jijini Dar Es Salaam hadi Dubai ambapo mtalala na kesho yake safari ya Qatar kuangalia mechi halafu tena mtarudi Dubai kutalii na kuangalia mazingira kabla ya kurejea nchini ” Alimalizia.

Naye kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya HISENSE Bwn. Joseph Mavura amesema kuwa kampuni ya Hisense inatoa ofa ya punguzo la 20% katika maduka yao yote na huduma ya kupelekewa huduma za bidhaa utakazonunua hadi nyumbani kwako BURE ( FREE DELIVERY ) kwa mteja atakayenunua bidhaaa na Kulipia kwa Tigo Pesa ” Alimalizia.

Naye mmoja wa Washindi wa Vifaa vya ndani ambavyo ni Tv inchi 50 , Friji , Microwave na Subwoofer kutoka chapa ya Hisense Bi. Rachel James Magongola Mkazi wa Bunju akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa Zawadi zake amesema kuwa.

” Kwakweli sikuamini kabisa , maana nlipigiwa simu na namba 100 ya Tigo na kuambiwa kwamba nimeshinda promosheni , nilifikiri ni matapeli lakini baadae nikaelekezwa kwamba ijumaa nifike hapa makao makuu kuchukua zawadi zangu na nimefika nimeziona zawadi zangu kwakweli sijui nisemeje lakini nawasihi watanzania msipuuze hii kampeni ya wakishua ni kweli kabisa , Fanyeni miamala kwa wingi maana zawadi bado zipo na sio vifaa vya ndani tu huenda labda naww ukaibuka mshindi wa safari ya kwenda Qatar kushuhudia mechi za kombe la dunia ukiwa umelipiwa kila kitu na Tigo ” Alimalizia .

Naye pia mmoja wa washindi wa Safari ya kwenda Qatar Bi. Clara Joseph amesema kuwa anafuraha sana kuwa mshindi na furaha yake kubwa ni kwenda kuwaona LIVE wachezaji wake pendwa wakicheza mpira ,

” Hakika hii ni furaha iliyoje , asante sana Tigo na Hisense mmefanya makubwa nawasihi Watanzania wafanye miamala kwa wingi huenda nao wakaibuka washindi kama ilivyotokeza kwangu maana sikutaraji ” Alimalizia Bi. Clara.