Na Joyce Kasiki,Timesmajira,Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa January 18 na 19 ambao pamoja na mambo mengine mrithi wa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara AbdulRahman Kinana atapatikana.
akizungimza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo Katibu wa Halmashauri Kuu Itikado Uenezi na Mafunzo wa CCM , CPA Amos Makala amesema Mkutano huo utatanguliwa na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa vikao ambavyo vitakutana Januari 16 mwaka huu ukiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano huo.
Aidha CPA Makalla amesema vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ndivyo vitapendekeza majina ya kupigiwa kura kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti huyo.
Amesema Agenda za mkutano Mkuu huo ni uchaguzi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambayo iliachwa wazi na Abdul-Rahman Kinana aliyejiuzulu mwaka jana,kupokea taarifa ya kazi za chama katika kipindi Cha 2022 Hadi 2025 na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar.
Makalla amefafanua zaidi kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti haigombewi isipokuwa inatokana na mapenedekezo ya vikao vya juu vya awali na baadaye kupigiwa kura za ndiyo na hapana katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi.
More Stories
Samia, Mwinyi wawapa miezi mitatu wawekezaji
Tanzania,Uingereza kushirikiana katika kuendeleza madini Mkakati
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi