LONDON, England
Harry Kane ameambiwa kuwa ni wakati wa kumalizia soka lake akiwa na Tottenham na kuhamia mojawapo ya vilabu viwili vya jiji la Manchester (Manchester City, Manchester United).
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza msimu huu alitajwa sana kujiunga na Manchester City lakini mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy alikwamisha dili hilo baada ya kumsaidia Pep Guardiola kunasa saidi ya Jack Grealish wa Aston Villa badala ya Kane.
Hata hivyo kutokana na uwezekano wa Spurs kutoingia tena kwenye nafasi ya nne bora msimu huu (Top 4 ya EPL), tetesi za Mshambuliaji huyo wa Uingereza kuondoka Spurs mwishoni mwa msimu huu zimeendelea kushika hatamu.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania