January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Harmonize kufanya ziara ya Muziki Marekani

Na Mwamdishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Kondegang, Rajabu Abdul maarufu kama ‘Harmonize’, ametangaza kufanya ziara ya muziki nchini Marekani kwa ajili ya kuutangaza mziki wake kimataifa.

Akitangaza ziara hiyo kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ambaye anatamba na ngoma yake ya
‘Sanadakalawe’amesema, ziara hiyo itaanza Agosti 28 mwaka huu huko Ohio na itafanyika ndani ya miji 15 nchini Marekani kwa kipindi cha miezi miwili.

Harmonize ambaye anatarajiwa kuachia albamu yake mpya iitwayo ‘High School’ hivi karibuni, ziara hii inakuwa ziara kubwa na ya kwanza kwa boss huyo wa Kondegang kuifanya nje ya nchi mwaka huu.