January 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Harmonize, Awilo kuachia wimbo wa ‘Attitude’ kesho kutwa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Kondegang, Rajab Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ April 23 mwaka huu, anatarajia kuuweka wimbo wake hewani ujulikanao ‘Attitude’ aliyemshirikisha mkongwe wa muziki wa dansi kutoka nchini Congo Awilo Longomba pamoja na msanii wa hapa nchini H. Baba.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake a Instagram Harmonize amesema, wiki hii wimbo wake huo utakuwa hewani hivyo wapenzi na mshabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea kazi yake ya nguvu.

“Siku ya Ijumaa April 23 mwaka huu, ninatarajia kuuweka hewani wimbo wangu ‘Attitude’a niliomshirikisha mkongwe wa muziki wa dansi Awilo Longomba pamoja na msanii nguli hapa nchini H. Baba,” amesema Harmonize.