December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hapi awaomba wananchi kuchagua viongozi wa CCM

Ashura Jumapili TimesMajira online Kagera,

Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Taifa,Ally Hapi,amewaomba wananchi wa Mkoa wa Kagera,kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa wanaotokana na chama hicho,unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Hapi,amesema hayo Novemba 20,2024,katika uwanja wa shule ya msingi Kashai iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Kagera kwa wagombea wa chama hicho.

Amesema viongozi wa Serikali za mitaa ni muhimu, kwa sababu mijadala yote ya maendeleo inaanzia huko na maendeleo yanahitaji muunganiko wa chama kimoja ambacho ni CCM.

Pia amesema wananchi wanao wajibu wa kuchagua chama hicho, kwa sababu Rais aliyeko madarakani anatokana na CCM na ni mwenye maono makubwa kwa taifa lake hususani kuwaletea wananchi maendeleo.

Amesema tangu Samia Suluhu Hassan, ameingia madarakani amejenga vituo vya afya zaidi ya 485 nchi nzima,vyenye uwezo wa kufanya upasuaji na kila hospitali ya Wilaya zimejengwa wodi maalum za wajawazito na watoto pamoja na majengo ya dharura kwa hospitali zote za mikoa.

Aidha amesema,amewekeza fedha za kitanzania kwenye treni ya umeme kiasi cha tirioni 23,ambayo itakuwa inabeba mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kupeleka Mwanza na nchi za Burundi. Congo na Uganda ikiwe ni sehemu ya ushindani wa bandari za nnchi jirani.

Hata hivyo amesema,vijiji zaidi ya 11,000 vimepatiwa umeme sawa na asilimia 97 na bado vijiji 480 ambavyo pia vipo kwenye mpango wa kupelekewa umeme.

Awali Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera , Nazir Karamagi,amesema ushindi kwa chama hicho ni lazima kwa sababu ya ajenda alizonazo Rais Samia Suluhu Hassan kwa taifa na Mkoa wa Kagera.Ambapo Mkoa wa Kagera una vijiji 662,vitongoji 3,664,Kata 192 na mitaa 66.

Karamagi,amesema amewawezesha vijana kujikwamua kiuchumi na msingi mzuri wa Rais ni serikali za mita na ndiyo msingi wa Serikali Kuu na kudai kuwa hakuna kitu kinaweza kufanyika bila wananchi kukubali.

Mbuge wa jimbo la Bukoba mjini Wakili Stephen Byabato,amesema wananchi wachague Chama Cha Mapinduzi ili Rais aendelee kuleta fedha nyingi za maendeleo kwa wananchi.

Wakili Byabato,amesema fedha zilizopokelewa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ni zaidi ya bilioni 60.

Vilevile amesema,miradi ya shule,hispitali na ujenzi wa vyumba vya madarasa zimetumika bilioni 17.9,maji bilioni 7, TARURA bilioni 4.4, hospitali ya rufaa Bukoba zaidi ya bilioni 5,bandari ya Bukoba bilioni 19,TANROAD zaidi ya bilioni 6 huku zaidi ya bilioni 18 ujenzi wa tawi la Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (UDSM). )