January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halmashauti Nkasi yatoa ufafanuzi wanafunzi waliofukuzwa shule

Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Nkasi


HALMASHAURI ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, imetoa ufafanuzi kuwa hayakuwa maelekezo ya Serikali ya kuwafukuza shule wanafunzi 9, tukio linalidaiwa kufanywa na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Izinga,Tarafa ya Wapembe Legiucy Martin Kawimbe.

Bali ni mgogoro kati ya Walimu na Wazazi, uliojitokeza Kijijini hapo,uliosababisha Mwalimu Mkuu kuwasimamisha shule wanafunzi hao na kuwataka wazazi wao wawatafutie shule nyingine.


Akitoa ufafanuzi juu ya jambo hilo mbele ya Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Afraha Hassan, amesema kuwa, Mwalimu Mkuu huyo alienda kinyume na utaratibu na wanafunzi hao wametejeshwa shule,hivyo hatua za kinidhamu zitachukuluwa pindi uchunguzi unaoendelea ikikamilika.

Amesema,kuna taarifa iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Izinga, kuwafukuza Wanafunzi 9 kama ni maelekezo ya Serikali,amedaiwa kuwa wazazi wa wanafunzi hao waliokuwa wamesimamishwa shule, waliwarushia matusi walimu wa shule hiyo baada ya kutokea kutoelewana,ndipo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo alipochukua uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi hao na kutaka wahamishwe shule hiyo waende shule nyingine.

Amedai kuwa hatua zilizochukuliwa za haraka ni kuwarejesha shule watoto hao bila ya masharti yote, kwani hatua alizochukuliwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ni kinyume na utaratibu na wameanzisha uchunguzi wa jambo hilo, na ikibainika kutenda kosa hilo hatua stahiki za kinidhamu na uongozi zitachukuliwa.Kwani kama mgogoro unawahusisha wazazi na walimu watoto hawahusiki kwa lolote.


Mkurugenzi Mtendaji huyo,amedai kuwa katika taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuwa maelekezo ya kuwafukuza watoto hao yalitolewa na Wizara ya Elimu kupitia,Mkuu wa Wilaya ya Nkasi hayana ukweli wowote bali ni migogoro yao tu.

Pia amedai kuwa Serikali itahakikisha wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, wanasoma bila kubughudhiwa wala kuingizwa katika migogoro yoyote ya kijamii na kisiasa.


Wanafunzi hao waliorejeshwa shule katika shule hiyo ni Mathias Sweetbeth Kabezya wa darasa la 3,Anakreda Sweetbeth Kabezya la kwanza,Grace Boniface Kabezya 4, Antonio Boniface Kabezya darasa la 4,Venus Boniface Kabezya darasa la 2 na Clephace Adabeth Kabezya darasa la 4.


Wengine ni Lilian Sweetbeth Kaswanya darasa la 5,Rosemary Sweetbeth Kaswanya darasa la 3 na Joseph Sweetbeth Kaswanya darasa la 2.