December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halmashauri zatakiwa kuboresha viwanja vya michezo shuleni

Na George Mwigulu,Timesmajiraonline, Mpanda.

MKUU wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mlindoko amewataka wakurugenzi katika halmashauri zote za mkoa wa Katavi kuhakikisha wanaboresha viwanja vya michezo shuleni ili kuendeleza vipaji katika sekta ya michezo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Akiongoza mbio za kilometa 5.10 na 21 Mkuu wa mkoa huyo amevitaka vyama vya michezo mkoa wa Katavi kuakikisha wanajipanga kusimamia mashindano ya ngazi zote.

Mrindoko ametaja changamoto ya ukosefu waviwanja vyenye ubora katika shule za Msingi na Sekondari nimiongoni mwasababu kubwa zinazo fanya vipaji vya wanafunzi wengi shuleni kudorora hivyo kuwa na vijana wasio kuwa na tija katika sekta ya michezo.

Akiwa miongoni mwa washiriki wa mbio za kilometa tano Mrindoko amesema kuwa wanakatavi wanapaswa kushiriki michezo kikamilifu ili kuongeza idadi kubwa ya watu wenye vipaji lakini pia kuondokana na magonjwa nyemelezi yanayo sababishwa na kutokuwa na mazoezi ya kutosha katika maisha ya kila siku.

Mrindoko ametoa zawadi kwa washindi walio shiriki mbio za kilometa 5.10 na 21 ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wa washiriki wakimichezo katika mkoa wakatavi .

Baadhi yawashiriki wa mashindano hayo ya michezo katika mkoa wakatavi wamejivunia kuwa miongoni mwa walio pata zawadi kama hamasa ya mashindano hayo lakini kuahidi kuboresha zaidi ili kuzidi kukuza sekta ya michezo katika mkoa wakatavi.

Ubora wa mashindano hayo ya michezo umekuwa fursa kwa baadhi ya washiriki wa mashindano hayo kwani baadhi yao wamepata kujisajili kuwa wanamichezo wakudumu ili kuendeleza sekta ya michezo na kuondokana na dhana potofu ya kuogopa kushiriki kwasababu za kujipatia kipato na kufanya kazi nyingine pasipo kutenga mda wa ziada katika kushiriki michezo

Mashuhuda wa mashindano hayo wamehaidi kuwa miongoni mwa watakao shiriki kamilifu na kujitoa katika kukuza sekta ya michezo na kuimarisha afya zao