Na David John, TimesMajira Online
HALMASHAURI ya Wilaya ya Temeke imezindua ujenzi wa viwanja vya michezo katika eneo la Mwembeyanga ambapo ujenzi huo unakwenda sambamba zoezi la kuipendezesha Manispaa hiyo.
Akizungumza na wandishi wa habari Jana wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam mkuu wa wilaya yaTemeke Jokate Mwegelo amessema kuwa ujenzi huo hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi milioni 998.
Amesema kuwa kwenye viwanja hivyo vya Mwembeyanga licha ya kujengwa viwanja vya michezo kama vile mchezo wa mpira wa miguu , mpira wa kikapu,mpira wa mikono kwa wanawake,na michezo mingine kama ngumi.
“Ndugu waandishi hapa Leo tumekuka kuzindua ujenzi ambao utakwenda zoezi la kuing’arisha Temeke kupitia tamko la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amoss Makalla ya kutaka kulifanya Jiji kuwa safi ” amesema Jokate
Nakuongeza kuwa “mradi huu pia utakwenda na zoezi la upandaji miti lakini kwa hapa viwanja vya mwembeyanga ,tutapanga bustani,tutaweka mauwa na lengo kupabadilisha madhari kuwa sehemu ya kivutio”amesema Jokate
Akizungumzia zaidi eneo hilo la Mwembeyanga mkuu huyo wa wilaya amesema ndani ya viwanja hivyo kutajengwa jengo la kumbukumbu la harakati za kudai uhuru ambayo (itaitwa Mwembeyanga Memorial) pia kutajengwa jengo la ofisi pamoja vyoo vya umma.
Pia ameongeza kutajengwa njia za kutembea kwa miguu ,maegesho ya magari na maeneo ya kufanyia biashara na pia kitakuwepo sehemu za wazi kwa ajili ya shughuli mbalimbali na itapandwa miti 93 mipya .hivyo aliwataka wakazi wa maeneo hayo kulinda miundombinu hiyo pindi itakapokamilika na Wakati mradi unatekelezwa.
Kwaupande wake mhandisi wa mradi huo ambaye pia ni mtumishi wa halmashauri hiyo ya Temeke Paul Mhere akizungumzia mradi huo alisema utaifanya Temeke kuwa ya kijani na kupitia ujenzi huo wa viwanja vya michezo maandalizo yote yamekamilika na tayari kazi inaendelea.
” Ndugu Mkuu wa wilaya niseme tu vifaa vyote vimekamilika na ujenzi wake unatarajia kukamilika ifikapo Agosti ,30 mwaka huu .”amesema
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini