Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema miongoni mwa vipaumbele vya chama hicho kwa wakazi wa Kalambo mkoani Rukwa ni pamoja na uboreshwaji wa miundombinu ya elimu, barabara na afya.

Dkt.Nchimbi ameyasema hayo Septemba 8,2025,uwanja wa Imbo, Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa,ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya kampeni akikinadi chama hicho kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi kukipigia kura CCM hkatika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Amesema, kati ya mambo yatakayofanyika katika Wilaya ya Kalambo ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya vitano na zahanati 16, shule za sekondari 5 zikiwa na idadi ya madarasa 30, pamoja na shule za msingi 6 zikiwa na madarasa 50.
Nyingine ni kuanzishwa kwa mradi wa maji safi utakao huduma vijiji 83 sawa na asilimia 92, ujenzi wa vizimba vya samaki zaidi ya 30, kuanzishwa kwa kituo cha ukuzaji wa viumbe vya majini katika Halmashauri hiyo pamoja na skimu za umwagiliaji nyingine ni uboreshwaji wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami na changarawe.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako