March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halmashauri ya Jiji Dar yapata hati safi

Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar

HALMASHAURI ya jiji la Dar es Salaam wamepata hati safi katika hesabu za fedha kwa Kipindi cha mwaka 2023 /2024 kwamujibu wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Charles Kichere.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kutoa taarifa ya Halmashauri hiyo Juni 18,2025  Kichera alipongeza kwa kupata hati safi huku akiwataka kuendelea kuwa na utendaji kazi mzuri zaidi .

Kichere,amesema Halmashauri hiyo ikiongozwa na Baraza la Madiwani na wataalam wake imeweza kusimamia vizuri Hesabu za Serikali.

“Katika Hesabu za mwaka 2023/ 2024 iliweza kupata hati inayoridhisha yaani hati safi,hivyo nampongeza Meya Omary Kumbilamoto, pamoja na Mkurugenzi wa jiji hili Eliuruma Maberya na Watendaji na Madiwani,”amesema Kichere.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert  Chalamila,amesema amemuhakikishia CAG kuwa watasimamia maagizo na maelekezo yote ambayo ameyatoa kuhakikisha Halmashauri zote zinafanya vizuri zaidi.

Katika hatua nyingine Chalamila amesema Madiwani wa Halmashauri hiyo mara baada Baraza kuvunjwa wiki hii  miezi mitano kabla kuunda Serikali mpya Mkurugenzi wa jiji ndio utakuwa Meya Watendaji wa Halmashauri ndio watakuwa Madiwani.

Aliwapongeza Ilala kwa makusanyo mengi kutoka bilioni 81 mpaka bilioni 130 ambapo aliwataka Ilala  waendelee kubuni kukusanya mapato mengi .

Meya Omary Kumbilamoto,amesema kwa niaba ya Madiwani wa Halmashauri walipata ushirikiano mkubwa kutoka Ofisi ya CAG na Ofisi ya Mkuu wa mkoa Dar es Salaam katika kutekeleza majukumu yao.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alisema wataendelea kukusanya mapato mengi na kufuata maelekezo ya CAG na maelekezo ya mkuu wa mkoa Albert Chalamila.