January 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Good hope yampa tano Rais Dkt. Samia

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Kikundi cha Vijana Wazalishaji Good Hope kilichopo Segerea Wilayani Ilala kinachojishugukisha kutengezea Gypsum na urembo kimeipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mikopo ya asilimia kumi ya Vijana na watu wenye ulemavu .

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mwenyekiti wa kikundi hicho Noti Hemed alisema kikundi chao kilianzishwa hivi karibuni na kilisajiliwa Mwaka 2022.

“Kikundi chetu kina wanachama sita walioajiliwa wapo 13 mikakati yetu kufikia Watumishi 25 Idara ya uzalishaji na masoko ” alisema Hemed.

Mwenyekiti wa Good hope Hemed alisema mikakati mingine ya kikundi hicho ni kufundisha Wanafunzi wa urembo mpaka sasa mradi umefikia asilimia 91.

Aidha alitumia fursa hiyo pia kuwapongeza viongozi mbalimbali waliowawesha kufikia malengo yao akiwemo Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus, Kamoli ,Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto ,mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ,Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri Diwani wa Segerea na Afisa Maendeleo Fransisca Makoye.

Mohamed alisema HALMASHAURI hiyo iliwapatia mkopo wa Shilingi milioni 180 ambapo kwa sasa wapo katika hatua kukamilisha taratibu za serikali Ili waweze kuzindua Ofisi yao.

Alisema awali kikundi chao kilikuwa na Changamoto mbalimbali baada kupata mkopo wa Serikali sasa hivi wameweza kufikia malengo yao kwa asilimia 91wanafanya Shughuli zao bila changamoto yoyote.

Aliwaomba wadau wa taasisi za Serikali na binafsi kuwa wateja wa bidhaa zao zitakapoingia sokoni Ili waweze kurejesha mikopo kwa wakati .