Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Video Vixen maarufu hapa nchini Gift Stanford maarufu kama ‘Gigy Money’, amewasamehe wale wote waliomtakia mabaya katika kipindi chote alichofungiwa kufanya kazi zake za sanaa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), lilimfungia miezi 6, Gigy Money kujihusisha na sanaa ndani na nje ya Tanzania na kulipa faini ya Tsh milioni 1, mara baada ya kupanda jukwaani mnamo Januari Mosi mwaka huu jijini Dodoma, akiwa amevaa dela kisha kulivua na kuonyesha mwili wake.
Akitoa msamaha huo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Gigy Money amesema, kama kuna mtu aliomba asifunguliwe, anamuombea kwa cMwenyezi Mungu ampe maisha marefu sana.
“Na kama kuna mtu alikua anaomba nisifunguliwe, basi namuombea kwa mungu Maisha Marefu sana. Na aibu yake ni yake kwani mimi nishawasamehe wote waliokua wananidhihaki, wananitukana wote nimewasamehe. Nataka kufanya mziki wangu bila makelele,” amesema Gigy Money.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio