January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gigy Money awajibu wanaomuona kapotea

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online

MSANII mwenye vituko vingi hapa nchini Gifti Stanford maarufu kama ‘Gigy Money’, amewajibu wale wote wanaomwambia kapotea kisanii na kuwaambia kuwa atapambana kuhakikisha anafikia malengo yake.

Akiwapa majibu hayo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Gigy Money amesema, kazi ya usanii haihitaji kuwa na pesa zaidi ya kupata sapoti kutoka kwa watu wako wa karibu kama ilivyokuwa nao yeye.

“Mimi kupendeza si utajiri. Kua msanii akuhitaji pesa kunahitaji supoti na watu wa karibu kama nilio nao mimi, wananishika mkono kila napokwama au kuanguka na kuhakikisha sikati tamaa katika ndoto zangu.Kwa hiyo nyie kuniona mimi napotea bado sana yani labda Mungu aamue, kwani nimebarikiwa mwenzenu,” amesema Gigy Money.