March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ghati achukua fomu kuomba ridhaa kugombea ubunge uwakilishi wanawake mkoa wa Mara

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Mara

Leo Juni 30, 2025, Mbunge aliyemaliza muda wake  wa viti Maalumu Mkoa wa Mara Ghati Zephania Chomete, amechukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kuwakilisha wanawake kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mkoa huo.

Ghati  Chomete amekabidhiwa fomu  hiyo Juni 30, 2025, makao Makuu ya CCM Mkoa  yaliyopo Mjini  Musoma  na  Katibu wa  Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Mkoa wa Mara Nderi Amos Isangya.