December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

GF Trucks & Equipment’s Ltd yawapiga msasa wachimbaji madini Chunya

Na mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wakati maonyesho ya madini yakifikia ukingoni kampuni ya uuzaji wa mitambo yamagari ya mizigo Gf Trucks & Equipment iliandaa semina elekezi kwa ajili ya wachimbaji wa madini na viongozi wa chama cha wachimbaji madini yenye lengo la kuwajengea uwezo

Maonyesho hayo ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika wilayani Chunya mkoani Mbeya yamefungua fursa kwa wafanyabiashara katika sekta hiyo ya madini kukutana na kuweza kubadilishana uzoefu kwani katika maonytsho hayo makampuni tofauti nchini yaliweza kushiriki na kubadilishana uzoefu na wachimbaji hao.

Akizungumza wakati wa semina elekezi Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks ,Smart Deus alisema wachimbaji wengi wanauwezo wa kukunua na hata kukodisha mitambo huduma ambayo inapatikana katika kampuni yetu ya GF lakini tatizo kubwa hawana uelewa wa kutosha katika uendeshaji kazi ambayo anaachiwa opareta wa mashine wakati mungine anaweza kumuongopea bosi kuwa Mtambo unatumia mafuta mengi kumbe ni uongo sasa kupitia semina hii tumeweza kuwaeleza namna bora ya kiitunza mitambo ili iweze kudumu muda mrefu na kuepukana na matatizo yanayoweza kuzuilika

Gf kwa sasa imefungua kiwanda cha kutengeneza maroli ya GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani kwa kutanua na kutumia magari ya FAW unaliongezea Taifa pesa kwani magari hayo yanatengenezwa nchini kwetu na sisi tunajivunia cha kwetu.

Pia GF hivi karibuni itafungua ofisi (yadi) katika mkoa wa Mbeya ili kuwasogezea huduma jirani wachimbaji kutoka ukanda wa nyanda za juu kusini kwa hiyo wateja wa Njombe,Chunya na Songwe wakae mkao wa kula wa kusogezewa huduma jirani hii ikiwa ni kutii maagizo ya mkuu wa mkoa wa Mbeya aliyetutaka kusogeza jirani huduma zetu.

GF pia ni wauzaji wa mashine za XCMG,AJAX, pamoja na maroli ya mizigo ya FAW na HONGYAN.

Akitoa neon la shukrani Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini mkoani Mbeya (Mberema) Leonard Manyesha alisema anawashukuru GF kwa kuweza kuwapa semina elekezi juu ya namna bora ya kutunza na kuisimamia mitambo yao katika shughuli za uchimbaji iliiweze kudumu kwa wakati na kuepuka kupata hasara zinazoweza kuzuilika Pia alisema wamefurahia kupata utaratibu rafiki kwa kuweza kukopa mmitambo hiyo kupitia mmoja ya benki kwa kutimiza mashari nafuu ambayo dhamana itakuwa mtambo wenyewe.

Naibu waziri wa Madini, Steveni Kiruswa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya wameutaka uongozi wa kampuni ya uuzaji wa Magari ya mizigo na Mitambo ya kuchimbia madini GF Trucks kuhakikisha wanafungua ofisi (Yadi) ya kuuzia mitambo jirani na migodi ili kuwafikia wahitaji kwa haraka.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Teknolojia ya madini yaliofanyika mkoani Mbeya katika Wilaya ya Chunya alizitaka kampuni zinazotoa huduma za kuuzaji wa vifaa mbalimbli vya migodini kufungua ofisi jirani ili kuweza kuwarahisishia wanunuzi ambao ni wachimbaji wadogo upatikanaji wa vifaa hivyo kwa wakati.

Akikazia kauli yiyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya aliiotaka GF Kuhakikisha wanachangamkia fursa ya kufungua ofisi jirani na machimbao hayo kwani kwa kufanya hivyo itarahisisha wao kukutana ana mteja mara kwa mara na sio kusubiri hadi wakati wa maonyesho.

Nae Meneja Masoko na Mawasiliasno wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd,Smart Deus aliseme wameipokea kama maagizo kauli hiyo ya viongozi na wanaamini muda sim mrefu watafungua ofisi katika maeneo hayo ili kuwa karibu na wateja wao.

GF & Equipment inajivunia kuwa wauzaji wa mashine za migodini (greda) aina ya XCMG,AJAX na magari ya mizigo aina ya FAW ambazo kwa sasa magari hayo ya FAW yanatengenezwa Kibaha mkoani Pwani Pia GF imefungua ofisi katika mikoa ya Mwanza,Geita Morogoro na Songea ilikujiweka karibu na wateja alimaliza Smart.

Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Mbeya(Mberema) ,Leonard Manyesha akipokea zawadi ya vifaa kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano GF Trucks & Equipment , Smart Deus kwa ajili ya kujikinga na vumbi pamoja na jua wawapo mgodini mara baada ya semina elekezi iliyooendeshwa na kampuni ya Gf wakati wa maonyeshobya madini yaliofanyika Chunya mkoani Mbeya.
Afisa Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Peter William akiwaezea ubora wa magari ya mizigo ya FAW kwa ajili ya matumizi ya migodini wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya Viongozi na wachimbaji wa madini wakati wa maonyesho ya Teknolojia ya Madini yaliofanyika Chunya mkoani Mbeya