November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Afisa Mauzo kutoka GCT, Mariam Matoloka akizungumza katika maonyesho ya 45.

GCAT yaleta sabuni za maziwa Sabasaba

Na David John, TimesMajira Online

MENEJA Mauzo kutoka Kampuni ya GCAT ambao ni wazalishaji wa bidhaa za afya na vipodozi salama, Mariam Matoloka ametoa rai kwa watanzania kupenda kutumia bidhaa za kiasili ili kuweza kuboresha ngozi ya mwili.

Amesema kuwa, bidhaa za kiasili zinafanya mwili kuwa safi na salama hususani kwa ngozi ya mwili, hivyo ni vema wananchi wakajenga mazoea ya kutumia bidhaa asilia.

Akizungumza katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba vilivyopo Barabara ya Kilwa wilayani Temeke, Meneja Mauzo Mariam amesema, wananchi waje kwenye maonyesho hayo na wafike kwenye Banda la Tabwa ili kupata bidhaa hizo.

“Hapa tuna sabuni za maziwa ya mbuzi ambazo zinafanya ngozi ya mwili kuwa safi na salama, lakini pia zinaondoa mikunjo katika mwili,zinakuweka mwili kuwa nyororo.Hivyo waje watumie, Sabasaba hii kupata bidhaa bora kabisa,”amesema.

Amefafanua kuwa, licha ya uwepo wao kwenye viwanja hivyo vya Sabasaba, lakini pia ofisi zao zipo Masaki jijini Dar es Salaam na Mbagala wilayani Temeke, lakini pia wanapatikana Kariakoo,Kinondoni,Mbezi na Tegeta.

Pia amesema kuwa, nje ya Dar es Salaam wanapatikana mikoa ya Mtwara, Tanga (Lushoto) na Morogoro ambapo amesema, sabuni hiyo ya maziwa ya mbuzi inaondoa muwasho, madoa katika ngozi.

Mariam ameongeza kuwa, sabauni hiyo inarudisha ngozi kwenye uasili wake kama imeungua na jua pia inasaidia hata watoto,inaondoa mapunye, mba na mambo mengine mbalimbali katika mwili hivyo wajitokeze kupata huduma hizo.