Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
UAMUZI usioyumba wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wa kukaribisha makampuni ya kimataifa yenye uwezo na uzoefu wa kusimamia na kuendesha shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) umetajwa kuwa ni moja ya sababu zilizowezesha TPA kutoa gawio la sh. bilioni 153.9 kwa Serikali.
Hayo yamesemwa na wadau mbalimbali nchini wliozungumzia gawio la sh. bilioni 153.9 kwa Serikali Kuu kwa mwaka 2023/24 lilitolewa TPA ambalo limevunja rekodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Raphael Maganga, alisema uwekezaji wa miundombinu bandarini umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi wa kiutendaji na hatimaye kupaisha mapato yake na hatimaye kutoa gawio kubwa kwa Serikali kuu kwa kipindi tajwa.
“Mifumo yake kisasa inasomana vizuri na ile ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) sambamba na ile taasisi zingine. Kwa gawio la sh. bilioni 153.9 si haba ni matokeo chanya ya uwekezaji na mchango mkubwa wa sekta binafsi,” alisema Maganga na kuipongeza mamlaka hiyo.
Amesema maono ya Rais Dkt Samia na uwezo wa menejimenti ya TPA kutafsiri maono hayo kwa vitendo yamechangia kuongeza ufanisi ikiwemo kuongezeka kwa mizigo inayopita bandarini.
“Idadi ya mzigo unaopinda katika Bandari ya Dar es Salaam umeongezeka kwa kipindi cha miaka hii mitatu, kwa nini maboresho makubwa yaliyofanywa yameweza kuvutia watumiaji wa bandari ya Dar es Salaa,” alisema Maganga.
Wakili na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, Dkt Tasco Luambano, alisema TPA imeweza kutoa gawio ambalo hakuna taasisi yeyote imetoa gawio mwaka 2023/24 imeweza kufika hata nusu yake.
Amesema gawio hilo limeweza kufunga kabisa midomo ya wakosoaji. “Niliwahi kuzungumzia faida zitakapatikana kutokana na Serikali kuwa karibisha washindani tofauti kuja kuendesha shughuli za bandari.
Gawio la TPA kwa Serikali kuu inadhirisha kuongezeka kwa ufanisi ambao unachangia kuongezeka kwa mapato,” alisema Dkt. Luambano.
Dkt Luambano amesisitiza kuwa Bandari kama lango kuu la Uchumi ameshauri wadau kutoka sekta binafsi kushirikiana na Serikali kuwekeza kwenye miundombinu ya reli na barabara ili kubiliana na uwingi wa mzigo kwenye bandari.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Godwill Wanga, mbali ya kuipongeza TPA kwa kuwa kinara kwa kutoa gawio nono kwa Serikali alisema hiyo ni ushuhuda kwa kuboreka kwa mazingira ya kufanya biashara na kuvutia uwekezaji hapa nchini.
“Juhudi kubwa zimefanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara yanakuwa rafiki na wezeshi kwa makapuni binafsi na mashirika umma kufanya biashara na uwekezaji,” alisema Dkt Wanga.
Serikali imepokea gawio la jumla ya shilingi bilioni 637 kutoka taasisi na mashirika 145 ambapo kati ya pesa hizo sh. 278 zilitolewa na taasisi zinazofanya biashara (Business entities) na sh.358 ni kutoka taasisi za udhibiti (Regulatories)
Akipokea gawio hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Dkt Samia alisema Serikali inataka kupokea gawio la kutosha kutoka kwa taasisi zote kuanzia mwakani na kuelezea matumaini yake kuwa anategemea TPA itatoa zaidi ya mara mbili kutokana na kushimiri kwa biashara.
Katika kufanya kazi kiushindani na kujiimarisha kibiashara, TPA imeingia mikataba ya kiundeshaji kwenye baadhi ya gati zake katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo Kampuni ya DP World kutoka Dubai inaendesha gati namba 4 hadi 7 gati namba 0 hadi 3 zinaendeshwa kwa pamoja kati ya Mamlaka ya Bandari na Kampuni ya DP World.
Mbali ya DP World, kampuni ya Adani International Ports Holding Limited ( AIPH) ya India inaendesha gati namba 8 hadi 11 zamani zilizokuwa zinaendeshwa na iliyokuwa kampuni ya kimataifa ya Tanzania International Containers Terminal Services (TICTS) ambayo mkataba wake wake uendeshaji ulimalizika.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa