March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gavu:CCM siyo chama cha msimu kama vingine

*Awaomba wanna Tarime kukupigia chama hicho kura

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

KATIBU wa NEC, Oganaizesheni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Issa Haji Gavu amesema, chama hicho ndio pekee kinachofanya kazi ya kuwahudumia wananchi wakati wote, tofauti na vyama vingine.

Gavu amesema hayo Agosti 31, 2025, alipokuwa akihutubia wakazi wa Nyamongo, Wilaya ya Tarime Vijijini, mkoani Mara.

Amesema, CCM ndiyo chama pekee kisichoenda likizo baada ya uchaguzi, tofauti na vyama vingine ambavyo ‘hufufuka’ wakati wa kampeni pekee.

“CCM si chama cha msimu. Tangu kiasisiwe hakijawahi kwenda likizo. Vyama vingine vipo kwa ajili ya kutafuta uongozi, sisi tupo kwa ajili ya kutatua changamoto za Watanzania, hivyo ni vyema wananchi mkaendelea kukiamini na kwenda kukichagua kwa mara nyingine.Ushahidi wa kazi kubwa ya chama unaonekana wazi kupitia mageuzi ya kijamii na kiuchumi yaliyofanywa katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema Gavu.

Amesema maendeleo yaliyofikiwa Tarime na nchi nzima ni kielelezo cha dhamira ya kweli ya chama hicho kubadilisha maisha ya wananchi.

“Nawaomba ifikapo Oktoba 29 mwaka huu kila mmoja ajitokeze kupiga kura na kuchagua wagombea wa CCM. Sifa na weledi wa Samia na Nchimbi kuongoza taifa hili hazina shaka,”.