Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
MGOMBEA Udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chanika,wilayani Ilala mkoani Dar-es-Salaam,Gaudance Kashoka, aeleza mikakati yake ya maendeleo atakayoitekeleza endapo atashinda katika uchaguzi mkuu Oktoba 29,2025.
Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni Kata ya Chanika,Jimbo la Ukonga Kashoka,amesema akipata nafasi hiyo ataanza na uboreshaji wa miundombinu ya barabara za ndani kwa kiwango Cha lami ikiwemo ya Meru,Masai wawili,Nguvu Kazi ,Virobo na barabara ya Kidugalo.
Pia ujenzi wa masoko ya kisasa Chanika kwa ajili ya kuwatafutia fursa wafanyabishara waweze kukuza uchumi.
Aidha amesema atashirikiana na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa nane ya Kata hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Sanjari na hayo amesema atahakikisha anasimia sekta ya elimu kwa kuhakikisha shukr mpya za msingi Tungini na Yongwe zinajengwa huku hospitali ya Nguvu Kazi Chanika inafanyiwa upanuzi na iweze kupandishwa hadhi.
Hata hivyo ameeleza namna ambavyo atasimamia vikundi vyote pamoja na makundi maalum waweze kupata mikopo na kukuza mitaji yao kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI