March 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

GAINI,BAKWATA Mwanza yafuturisha wenye uhitaji

Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza

Kampuni ya GAINI kwa kushirikiana na BAKWATA Mkoa wa Mwanza,wamewafuturisha waumini wa dini ya Kiislamu mkoani hapa huku wito ukitolewa kwa wenye uwezo kiuchumi kufuturisha watu wenye mahitaji katika jamii.

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hassani Kabeke,amesema wakati wa Ramadhani, watu wenye uwezo kiuchumi na taasisi ni vyema zikafutirisha watu wanoishi katika mazingira magumu pamoja na yatima, wajane, maskini,wanafunzi,wafungwa na  mahabusu waliopo magereza.

Meneja wa kampuni hiyo tawi la Mwanza,Shabaani Mapande, amesema mbali na futari wametoa  vyakula anuwai ikiwemo mchele, maharage, sukari na mafuta ya kupikia kwa shule ya sekondari Sengerema, vituo vya kulea watoto yatima,wajane na masikini.

“Tunafanya haya kurejesha fadhila kwa jamii kwa tulichokipata ambapo vyakula hivyo vimetolea kwa makundi mbalimbali ya wanaoishi katika mazingira magumu viwasaidie kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani,”.

 Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine, amesema,”Tumezoea kufuturisha Gold Crest, Malaika na kwingineko.Hapa tunapata pia thawabu inayowagusa watu wenye mahitaji maalum, watoto wanafurahi na hivyo Mwenyezi Mungu akinijalia nitafanya jambo siku chache zijazo,”amesema.

Sima amesema kwa kutambua umuhimu wa vituo vya afya vinavyojengwa na BAKWATA ili kuunga mkono jitihada za Sekarikali za kuboresho sekta ya afya, alichangia shilingi 500,000,