Na Nuru Mkupa, TimesMajira Online, Dodoma
UONGOZI wa Kituo cha Kukuza na Kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali cha Fountain Gate kilichopo jijini hapa kimedhamiria kufanya mapinduzi makubwa ya kimichezo.
Baadhi ya mikakati iliyopo mbele yao ni kuhakikisha wanaendelea kutoka mafunzo ya mchezo wa Soka kwa vijana wa kike na kiume na kuipandisha timu yao inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Pia wamedhamiria kujikita katika mambo mengine ikiwa ni pamoja na kukuza na kuendeleza Sanaa mbalimbali ambazo kwa pamoja zitawaleta karibu vijana na kufanikisha malengo ya kituo hicho ambacho hadi sasa kina timu za vijana chini ya umri wa miaka 20, chini ya miaka 17 chini ya miaka 15, timu ya wasichana pamoja na timu yao ya FDL.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Wendo Makao ameuambia Mtandao huu kuwa, pamoja na mikakati hiyo ambayo ipo mbele yao, kituo chao kinazingatia uwepo wa Elimu bora na uendelezaji wa vipaji na anaamini kutokana na juhudi zinazofanywa na uongozi, baada ya kipindi kifupi kutakua na mafanikio ya kimichezo ndani ya Dodoma na Taiga kwa ujumla.
“Kituo chetu kwa ujumla kinafuata taratibu zote pamoja na misingi bora ya uendelezaji wa vipaji hivyo naamini kwa kasi tunayoenda nayo, tutafanikiwa kuleta maendeleo ya kimichezo kwani umoja na mshikano baina ya wafanyakazi, wanafunzi pamoja na bodi ya kituo ni vitu ambayo tunajivunia sana katika kufanikisha haya tuliyoyakusudia,” almesema Mkurugenzi hiyo.
Kwa upande wake, Ofisa Habari na Mawasiliano wa timu ya Fountain, Juma Ayo amewaomba wapenzi wa Soka katika jiji hilo, kuiunga mkono timu yao kuelekea kwenye msimu mpya wa FDL utakaoanza rasmi Oktoba 9.
Katika ufunguzi wa Ligi hiyo, Fountain Gate itakuwa nyumbani katika uwanja wa Jamhuri kuwakalibisha Alliance FC kutoka Mwanza.
Ayo amesema kuwa, kikosi chao kimejipnga vizuri kwa ajili ya kutafuta alama tatu muhimu kwenye mchezo na tayari wameshacheza mechi kadhaa za kirafiki ikiwemo dhidi ya JKT Tanzania na Mawenzi Market ya Morogoro ikiwa ni maandalizi kuelekea Ligi hiyo.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania