November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

KAMISHINA wa maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma Jaji Harold Nsekela. (Picha na Joyce Kasiki)

Fomu za maadili ya viongozi sasa kujazwa kimtandao

Na Joyce Kasiki

KAMISHINA wa maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma, Jaji Harold Nsekela amesema hivi sasa fomu za maadili ya viongozi wa umma zinajazwa katika mtandao badala ya kutumia makaratasi kama ilivyokuwa awali.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dodoma, Jaji Nsekela amesema kuwa, mfumo huo utawarahisishia viongozi wa umma kujazwa fomu za Mali na madeni yao bila kutumia gharama.Ametumia firsa hiyo kuwataka viongozi wa umma kujaza fomu hizo kwani ninsuala la kikatiba.

“Bado kuna viongozi wanadhani kujaza tamko hili ni ombi ,hili siyo ombi,maana kama Rais mwenyewe anajaza viongozi mwingine ni nani hadi asijaze” alisema Jaji Nsekela Amesema,kwa viongozi wanaohitimisha uongozi wao katika utumishi wa umma dirisha linafunguliwa oktoba mwaka na kufungwa Desemba 31  mwaka huu.

Vile vile amesema, kwa watumishi wapya wanapaswa kujaza fomu hizo ndani ya Siku tangu walipoajiriwa.Ujazaji wa fomu za Mali na madeni kwa viongozi wa umma umekuwa ukifanyika kwa njia ya kuandika kwa mkono na kutumia kwa njia ya posts lakini sasa zoezi hill linafanyika kwa njia ya mtandao ambapo humwezesha viongozi kujaza fomu hiyo popote atakapokuwa na bila usumbufu wowote.