November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

FIFA yatoa orodha fupi wachezaji bora Wanaume, Wanawake 2020

ZURICH, Uswiss

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), limetoa orodha fupi za Mchezaji Bora wa Wanaume na Wanawake wa miezi 12 iliyopita, pamoja na kocha bora wa mwaka 2020.

Hiyo imekuja baada ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka (Ballon d’Or) ya 2020 kufutwa na mratibu wa Soka la Ufaransa, ikimaanisha kuwa FIFA itasimamia tuzo za hadhi za juu zaidi ulimwenguni mwaka huu.

Walioteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Wanaume wa FIFA 2020 ni, aliyeshinda mwaka jana Lionel Messi pamoja na watatu wa Liverpool Mohamed Salah, Virgil van Dijk na Sadio Mane. Messi ameteuliwa kwa mara nyingine tena kama mpinzani wake Cristiano Ronaldo na Nyota wa Bayern Munich Robert Lewandowski.

Mchezaji Bora kwa upande wa Wanaume wa FIFA:-

Thiago Alcantara (Uhispania / Bayern Munich / Liverpool)

Cristiano Ronaldo (Ureno / Juventus)

Kevin De Bruyne (Ubelgiji / Manchester City)

Robert Lewandowski (Poland / Bayern Munich)

Sadio Mane (Senegal / Liverpool)

Kylian Mbappe (Ufaransa / Paris Saint-Germain)

Lionel Messi (Argentina / Barcelona)

Neymar (Brazil / Paris Saint-Germain)

Sergio Ramos (Uhispania / Real Madrid)

Mohamed Salah (Misri / Liverpool)

Virgil van Dijk (Uholanzi / Liverpool).

Mchezaji Bora kwa upande wa Wanawake wa FIFA:-

Lucy Bronze (England / Lyon / Manchester City)

Delphine Cascarino (Ufaransa / Lyon)

Caroline Graham Hansen (Norway / Barcelona)

Pernille Harder (Denmark / Wolfsburg / Chelsea)

Jennifer Hermoso (Uhispania / Barcelona)

Ji So-yun (Korea Republic / Chelsea FC Wanawake)

Sam Kerr (Australia / Chelsea)

Saki Kumagai (Japan / Lyon)

Dzsenifer Marozsan (Ujerumani / Lyon)

Vivianne Miedema (Uholanzi / Arsenal)

Wendie Renard (Ufaransa / Lyon).

Kocha Bora kwa upande wa Wanaume wa FIFA:-

Marcelo Bielsa (Argentina / Leeds United)

Hans-Dieter Flick (Ujerumani / Bayern Munich)

Jurgen Klopp (Ujerumani / Liverpool)

Julen Lopetegui (Uhispania / Sevilla)

Zinedine Zidane (Ufaransa / Real Madrid)