Wazir Junior aliyekuwa mchezaji wa Mbao FC na sasa ni mchezaji wa Yanga ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Julai. Kwa upande mwingine Fred Felix Minziro wa timu hiyo ametwaa tuzo ya kocha bora kwa mwezi Julai.
Wazir Jr kwa sasa ni mali ya Yanga na alisaini mkataba utamweka klabuni hapo mpaka mwaka 2023.Wazir alikuwa na msimu mzuri kwa 2019/20 huku akifunga mabao 13 na kumfanya awe kinara wa mabao kwa Mbao FC jambo lililowavutia mabosi wa Yanga kumsajili
Mbali na Mbao FC kushindwa kubaki ligi kuu baada ya kutolewa kwenye play off lakini ni yeye aliyefunga mabao mawili kati ya 4-2 walizoshinda mechi ya kwa kwanza.
Wazir ametwaa tuzo hiyo baada ya kucheza mechi 6 za ligi kwa mwezi julai huku akifunga mabao matano na kutoa pasi ya bao moja kigezo kilichomfanya aibuke kinara mbele ya Obrey Chirwa wa Azam na Peter Mapunda wa Mbeya City.
Hii inakuwa ni tuzo ya pili kwa Wazir Junior kutwaa kwa msimu wa 2019/20 baada ya kushinda tuzo bora ya mchezaji bora mwezi November 2019.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM