Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Taasisi ya Foundation For Disabilities Hope (FDH) imeanza kuteleza mradi wa mwaka mmoja wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu kushiriki masuala ya uongozi pamoja na ujasiriamali ili kuwainua kiuchumi.
Mradi huo wa mwaka mmoja unalenga kuwafikia wanawake wenye ulemavu zaidi ya 300, katika kata mbalimbali za Halmshauri ya wilaya ya Kondoa.
Mkurugenzi Mtendaji wa FDH, Maiko Salali, akizungumza wakati wa utoaji wa mafunzo
wilayani kondoa, amesema mradi huo wa mwaka mmoja umejikita kusaidia watu wenye ulemavu kukamata fursa za kiongozi pamoja na ujasiriamali.
Alisema takwimu zinaonyesha ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye masuala ya uchanguzi mbalimbali nchini bado ni hafifu hali ambayo inahitaji jitihada za pekee kuibadili.
“Hata katika uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa hivi karibuni takwimu zinaonyesha kuwa ushiriki wa wa watu wenye ulemavu ulikuwa mdogo sana lakini pia hata ushiriki wa wanawake ulikuwa hafifu sana hivyo ipo haja kwa wadau pamoja na serikali kuweka jitihada kubadili hali hii.
“Tutakua hapa kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuwaelimisha na kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu waweze kushiriki kikamilifu katika michakato mbalimbali ya kiuongozi niwashukuru sana Abilis Foundation kwa kufadhili mradi huu ili kuongeza elimu na uelewa kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu ili kuwa na jamii jumuishi”amesema
Aidha, amesema wanaishukuru wilaya ya Kondoa kwa kutupatia ushirikianao ili kuwafikia na kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu ili mtu mwenye ulemavu asonge mbele.
Ofisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Kondoa Jafari Haji, alisema mradi huo umekuja wakati mwafaka kwani watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na chanamoto mbalimbali ikiwemo ushiriki wa masula ya uongozi.
“Mafunzo ambayo yanayotolewa kupitia mradi huu yatasaidia watu wenye ulemavu kushiriki kwenye masula mbalimbali yakiwemo ya kiungozi pamoja na ujasiriamali”amesema
Salma Ramadhani, mkazi wa Kondoa ameshauri wazazi kuacha kuacha tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu bali wawatoe ili wapate haki zao za msingi ikiwemo elimu.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa