Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
SERIKALI imekutana na Wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nchini kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote haswa mizigo hiyo kuwa na Nembo ya nchi zilipozalishwa ili kuondokana na matatizo ya bidhaa bandia.
Akizungumza na waandishi Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio amesema kuwa ni muhimu kwa Wafanyabiashara kufanyabiashara kwa kuzingatia matakwa ya sheria.
“Nia yetu kufanya Biashara katika Mazingira Mazuri ili kuwezesha makampuni kuweza kulipa kodi”. amesema Erio.
Aidha, Erio amesema kuwanivyema bidhaa inayoingizwa nchini ijulikane inatoka wapi, ili kuweza kujua bidhaa inatoka wapi endapo itajulikana ina matatizo. “Sheria inataka Mzalishaji wa bidhaa Anuani yake inatoka wapi”.aliongeza
Kwa upande wake Mzalishaji wa spea za pikipiki wa kampuni Wuhua Huang amesema kuwa ameiomba seikali kuweza kutengeneza Mazingira ya uagizaji wa bidhaa kwa pamoja ikiwemo tume ya ushindani kujenga fursa mbalimbali kwa wafanyabiashara kukaguliwa bidhaa zao kwa pamoja kupitia tume hiyo.
Naye Mkurugenzi wa udhibiti wa Ubora Khadija Ngasongwa amesema ni muhimu kwa wasambazaji wa bidhaa wakajiridhisha kuwa bidhaa hiyo inakidhi viwango kabla ya kuwauuzia wengine.
Hivyo, amesema kumekuwa na changamoto ya Asili ya bidhaa ya cement wakati wa kutathimini ubora kipindi cha uhitaji, “Sheria inataka bidhaa hiyo ioneshe inatoka wapi “. amesema Mkurugenzi wa udhibiti ubora Khadija Ngasongwa.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria