January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Fani ya useketaji mkombozi wa ajira nchini

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MWALIMU wa fani ya useketaji (utengenezaji wa vitambaa vya nguo,vikoi) chuo cha VETA Tabora  Diana Mlengeki amewaasa vijana kusoma fani ambazo siyo maarufu kwani ndio fani zenye fursa kubwa ya ajira.

Mwalimu Mlengeki ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandiahi wa habari kwenye banda la VETA kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (88).

Amesema vijana wengi wamekuwa wakikimbilia kusoma fani ambazo ni maarufu kama vile ufundi wa magari,umeme na fani nyingine mwisho siku inaendelea kuketa changamoto hata soko la ajira za kujiari.

Amesema fani kama ya  useketaji  ambayo inafundisha kutengeneza vitambaa vya aina mbalimbali kwa kutumia nyuzi za pamba au nyuzi zozote haina umaarufu lakini ina fursa kubwa ya ajira hata za binafsi.

“Vijana wengi wanakimbilia kujifunza fani za umeme au magari ambazo nibfani maarufu kwa hiyo unakuta hata ajira ikutangazwa inahitaji watu wawili lakini waombaji wanakuwa hata zaidi ya 1,000,sasa hii ni changamoto.” Amesema Mwalimu huyo

Mwalimu Mlengeki amesema,katika chuo hicho wana mashine ndogo na mashine kubwa ambapo unaweza kutengeneza ‘table mart’ na mitandio ambapo  mashine kubwa hutumika kutengeneza vitambaa vya kushonea magauni au mashati na vikoi .

Amesema wao wamelenga kufundisha vijana wa kitanzania ili waweze kujiajiri huku akisema kama viwanda vya hapa nchini  vya nguo na nyuzi vingekuwa vinafanya kazi vizuri basi wabaotoka VETA ndio wangekuwa wataalam katika viwabda hivyo.

Amesema mashine ndogo inapatikana kwa  150,000 na inaweza kutengeneza mitandio miwili kwa siku ya mita mbilimbili na mashine kubwa ambayo huuzwa kwa  milioni 1.5 hutengeneza mitandio  hadi 7  kwa siku.