January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

KWA TAARUFA YAKO :Masabuni alinusurika kifo katika Meli ya Titanic

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online


Masabumi Hosono aliyeishi duniani kati ya mwaka1870 hadi 1939, ndiye raia pekee wa Japan aliyenusurika kifo katika ajali ya meli maarufu ya Titanic.

Aliporejea nchini kwake baada ya ajali, alikuwa akilaumiwa na kudharauliwa na kila Mjapani kwa kujiokoa yeye binafsi na kushindwa kuokoa wengine.

Wajapan walikuwa wakimuona Hosono kuwa ndiye Mjapani muoga zaidi kuliko wote nchini humo.

Meli kubwa ya Titanic ilizama kwenye Bahari ya Atlantic Aprili 5, 1912 ikiwa ni siku nne baada ya kuanza safari yake kutoka Southampton nchini Uingereza kwenda New York nchini Marekani.

Na ilisababisha vifo vya watu 1,500 kati ya 2,224 waliokuwemo kwenye meli hiyo, huku mali za watu zikiharibika.

Kuzama kwa meli hiyo kulitokana na kugonga kwenye mwamba wa barafu.