Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online Mwanza
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendesha mafunzo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuwafahamisha kuhusu kazi,wajibu na mafanikio ya EWURA katika udhibiti wa huduma za nishati na maji.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Jumatatu Februari 1,2021 na kukutanisha waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mara, Geita na Simiyu katika ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza ambapo wamepata fursa ya kufahamishwa kuhusu kuanzishwa kwa EWURA, sekta inazozitawala, muundo wake, mafanikio na changamoto zake.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Godfrey Chibulunje amesema waandishi wa habari ni wadau wakubwa wa EWURA katika utendaji wao wa kazi na kwamba wanafanya kazi kwa uwazi na mara nyingi wamekuwa tayari kutoa ufafanuzi kwa jambo lolote lile ambalo waandishi wa habari wanahitaji ili kuihabarisha na kuielimisha jamii.
Chibulunje amesema EWURA itaendelea kutoa ushauri kwa serikali katika kuandaa sera,sheria na kanuni zitakazowezesha kukua kwa sekta za nishati na maji na kuendelea kusimamia watoaa huduma ili kuhakikisha huduma zinakuwa bora kwa manufaa ya taifa.
Aidha, amesema EWURA imesaidia kuzuia mfumko wa bei, kuimarisha mamlaka za maji nchini na kukuza umeme binafsi na kwamba itaendelea kuzingatia misingi mikuu sita ya utawala bora katika maamuzi ya udhibiti ambayo ni weledi, uwajibikaji, utabirikaji, ushirikishaji, uwazi na kufuata sheria.Â
Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina amewaomba waandishi wa habari kuendeleza ushirikiano walionao kwa EWURA nao wataendelea kutoa ushirikiano.
Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza, Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa kuandaa mafunzo hayo na kuahidi kuwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa wataendelea kushirikiana na EWURA.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best