July 31, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

EWURA yawajengea uwezo Maafisa kuboresha huduma wateja

Na Mwandishi wetu,Babati, Manyara

MAMLAKA  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini imeendesha semina ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Huduma kwa Wateja, Mahusiano na Sheria kutoka TANESCO na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Kanda ya Kaskazini kuhusu huduma kwa wateja na uzingatiaji wa matakwa ya kisheria.

Akifungua semina hiyo katika katika mji wa Babati, Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini,  George Mhina, aliwasisitiza washiriki kuyafahamu vyema majukumu yao ili waweze kutoa majibu sahihi, ya wakati na yanayozingatia sheria, hivyo kuboresha huduma kwa wateja.

Kwa niaba ya washiriki, Devotha Mayala kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga na Bw. Samwel Mandari kutoka TANESCO waliishukuru EWURA kwa mafunzo hayo, wakieleza kuwa yamewaongezea uelewa na uwezo wa kuwahudumia wateja kwa weledi zaidi.

Semina hiyo ni sehemu ya juhudi za EWURA za kuimarisha uwezo wa watoa huduma na kulinda haki za watumiaji wa huduma za nishati na maji kupitia Udhibiti wa Haki kwa Matokeo Chanya.