Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za petroli zitakazotumika nchini hapa,kuanzia Jumatano Agosti 6, 2025, zikionesha kupungua kwa bei ya petroli kwa shilingi 34 kwa mafuta yaliyopokelewa bandari ya Dar-es-Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile, imeeleza kuwa bei ya petroli katika soko la dunia imepungua kwa asilimia 2.3, huku dizeli ikiongezeka kwa asilimia 5.7 na mafuta ya taa kwa asilimia 3.7.
Vilevile, taarifa hiyo imebainisha kuwa viwango vya kubadilisha fedha,kwa bei za mwezi Agosti 2025, wastani wa gharama za kubadilidha za kigeni umepungua kwa asilimia 2.
Kwa upande wa ghama za kuagiza mafuta, kwa Bandari ya Dar-es -Salaam zimepungua kwa wastani wa asilimia 12.3 kwa petroli,asilimia 3.11 kwa dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa asilimia 13.08,bandari ya Tanga kukiwa hakuna mabadiliko huku kwa bandari ya Mtwara gharama zimeongezeka kwa asilimia 6.12 kwa mafuta ya petroli na asilimia 60.82 kwa dizeli.
Aidha, EWURA imewakumbusha wafanyabiashara kuuza mafuta kwa bei zilizoidhinishwa na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi