Na Mwandishi Wetu
BEI ya mafuta ya Oktoba, mwaka hii itaendelea kutumika kwa mwezi Novemba baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kutangaza bei ya kikomo ambayo haijafanyiwa marekebisho yoyote.
Bei hiyo iliyotangazwa itahusu mafuta yote yanayopita katika bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.
Taarifa ya Ewura iliyotolewa jana inaonesha kuwa sasa wakazi wa Dar es Salaam watanunua lita moja ya petroli kwa sh, 2,752 sawa na iliyokuwa ikitumika Oktoba mwaka huu.
Kwa watumiaji wa dizeli wataendelea kutumia sh.2,704 kwa lita moja ya mafuta kama ilivyokuwa Oktoba na mafuta ya taa wakiendelea kutumia sh. 2,774 kwa lita.
Kwa wanunuaji wa rejareja kwa mafuta yanayopita Bandari ya Tanga sasa watanunua petroli lita moja kwa sh. 2,813, dizeli Sh2,766 huku mafuta ya taa yakisalia sh. 2,835.
Kwa Bandari ya Mtwara, petroli itaendelea kununuliwa kwa sh. 2,844, dizeli kwa sh. 2,797 na mafuta ya taa yakiendelea kusalia kwa sh.2,866 kama ilivyokuwa Oktoba mwaka huu.
Taarifa hii iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Ewura, Dk James Mwainyekule eendelea kuvitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika.
“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.
Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja,” ilisema taarifa hiyo.

More Stories
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini
REA imeleta mageuzi sekta ya nishati