Na Penina Malundo
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo amepokea msaada wa hundi ya kiasi cha Shilingi. Milioni 100 kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) iliokabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Godfrey Chibulunje.
Aidha, Waziri Ummy amepokea msaada wa ndoo 480 sawa na Lita 9600 za vitakasa mikono (Hand Sanitizer) zenye thamani ya Shilingi. Milioni 11 zilizotolewa na kampuni ya Mafuta ya Mount Meru ambazo zitatumika katika kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini. Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma, Waziri Ummy ameshukuru kupata misaada hiyo ambayo itasaidia katika kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini na pia amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari licha ya maambukizi ya ugonjwa huo kupungua nchini
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote