Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Tabora
KAMPUNI ya ETDCO imeendelea kujenga miundo mbinu ya kusafirisha umeme nchini ikiwemo njia ya kutoka Tabora hadi Katavi, ambapo njia hiyo ya kusafirisha umeme na tayari umefka asilimia 67.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja Mkuu Kampuni ya ETDCO, CPA Sadock Mugendi wakati aliokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme mkoani Tabora.
ETDCO ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania na ni suluhisho la miundo mbinu ya umeme kwani ipo kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundo mbinu ya kusafirisha na kusambaza umeme.
Mugendi amesema kuwa mradi wa kutoka Tabora kwenda Katavi wenye urefu wa kilometa 383 wa msongo wa 132kv ambao unatarajiwa kumalizika mwaka huu na kupelekea Mkoa wa Katavi kupata umeme wa uhakika pia kuipunguzia gharama TANESCO za kununua mafuta ya dizeli kwajili ya jenereta ili kuzalisha umeme kwenye Mkoa Wa Katavi.
CPA Sadock ameipongeza serikali kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya Nishati ili kuhudumia wananchi wake vizuri, amesema hayo wakati akitembelea mradi wa kimkakati wa Tabora kwenda Katavi wenye msongo wa 132kV.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba