Na Penina Malundo,Timesmajira
VIJANA takribani 40 kutoka vyama mbalimbali nchini wameweza kuwajengea uwezo katika masuala ya demokrasia na mchakato wa mzima wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba Mwaka huu.
Vijana hao wametakiwa kuondoa hofu,kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu,kugombea na kutengeneza hoja za kuwashawishi wananchi kuweza kupigiwa kura pindi mchakato huo utakapoanza.
Ameyaasema hayo jana jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Mazingira na Haki za Binadamu(ENVIROCARE),Amos Mbwambo amesema Vijana kwa sasa wanaonesha kujiamini tofauti na miaka ya nyuma kwani wamekua wakitoka mbele na kugombea nafasi mbalimbali katika vyama vyao.
Amesema mbali na kujitokeza pia wamekuwa wanajieleza vizuri wakati wa kuomba kura na kunadi sera zao,hii ni ishara ya kuonesha kuna maendeleo mazuri kwa ushiriki wao katika chaguzi mbalimbali.
Mbwambo alisema tayari baadhi ya vyama vijana wamefanya vizuri katika chaguzi zao za ndani hivyo wanategemea kuona vijana wengi zaidi katika uchaguzi mkuu Oktoba 2025.
”Mafunzo haya ni muendelezo ya mafunzo ya awali ambayo tuliyatoa Agosti,2024 na yaliweza kuleta matokeo chanya katika Chaguzi za Serikali za Mitaa,mradi huu umekuja baada ya kupata matokeo mazuri ya mradi uliopita ambapo huu utakuwa wa miezi 21 hadi Agosti 2026.
”Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Forum CIV kutoka nchini Sweeden ambapo unatekelezeka katika wilaya tatu Ubungo,Kinondoni na Kigamboni wenye lengo la kuondoa changamoto iliyopo kwa vijana na wanawake kwa kuwa nyuma kwenye masuala ya uongozi,”amesema
Kwa Upande wake,Godlisten Murro Meneja wa miradi katika Shirika hilo,amesema walianzisha mradi huu baada ya kufanya utafiti na kubaini kwamba wanawake wengi na vijana wengi hawashiriki katika masuala ya uongozi.
Amesema waliweza kubainisha mambo mbalimbali ambayo yanawakwamisha wanawake na vijana kuweza kujihusisha na uongozi.”Tulibaini Changamoto zinazowakumba sana vijana ni pamoja na suala la mila na desturi ambapo watu wengi wanaamini hawawezi kuongozwa na wanawake,wengine wanaamini vijana hawana busara hivyo wengi kuchagua wazee wakiamini kwamba wazee ni watu wenye busara.
Naye Katibu wa Bavicha Jimbo la Kibamba,Nice Sumari amesema mafunzo hayo yamekuwa na mchango mkubwa kwa vijana ambapo yamewapa chachu ya kuleta mabadiliko kwa vijana wengine kwenda kugombea katika serikali za mitaa.
Denis Ngonyani Mjumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Uvccm Ilala,amesema Chama chao cha CCM kinamifumo ya kuwatengeneza vijana wajibu wa kuendelea kushika madaraka.”Kwetu sisi vijana hatukuwa tunaonekana sana ila tulikuwa tunajipa muda ya kusikiliza viongozi waliotutangulia ambao wao ndio misingi wa kujua nchi imetoka wapi.
More Stories
Serikali yaboresha sekta ya elimu Ulyankulu
Sababu za matukio ya ukatili zatajwa
Upungufu wa maji Mji Korogwe, HTM waeleza mikakati yao