Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa(UN),limeeleza kuwa kila sekunde 24, mtu mmoja anapoteza maisha kwa ajali ya barabarani huku nchi za kipato cha chini na kati ndiko zaidi ya asilimia 90 ya vifo vitokanavyo na ajali barabarani hutokea.
Ili kupunguza ajali za barabarani na majini elimu inapaswa kuendelea kutolewa kwa jamii pamoja na kubadili mtazamo na fikra wakati wanapotumia vyombo vya moto wa wapo safarini au barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari,Katibu Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Uzalendo Wetu Safarini barabarani na majini,Kalembe Henry,walipotembelea ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), ameeleza kuwa ajali za barabarani na majini zimekuwa changamoto nchini huku zikiacha watu wakiwa na ulemavu majonzi baada ya wapendwa wao kupoteza maisha na kuchangia umaskini kwenye familia.
Kalembe, ameeleza kuwa ili kuhakikisha ajali hizo zinapungua kama wazalendo waliamua kuanzisha shirika hilo ili kuelimisha jamii kubaini mazingira hatari ya vyanzo vya ajali na kutoa ushauri wa haraka kwa ajili ya kudhibiti ajali za barabarani na majini.
“Watanzania kuwa wazalendo na kubadili fikra na mitazamo wawapo safarini ili kukomesha ajali za barabarani na majini kwa kupaza sauti endapo kutakuwa na ukiukwaji wa sheria barabarani na majini zinazoweza kusababisha ajali endapo hazitafuatwa,”ameeleza Kalembe.
Hata hivyo ameeleza kuwa lengo la shirika hilo ni kuwaelimisha watu waweze kujiepusha na ajali baada ya kuona watu wengi wanaangamia kutokana na ajali zinazotokana na sababu mbalimbali barabarani na majini.
“Ni vyema jamii ya watanzania bara wakapata elimu ili kubadili fikra na mitazamo yao na waweze kuepuka ajali kwa kuambikizana tabia ya uzalendo,kwani tunapotoa elimu ya usalama barabarani na majini itawasaidia wao na vizazi vijavyo,”ameeleza.
Kwa upande wake Mjumbe wa shirika hilo,Musa Ipuli, ameeleza kuwa jamii ikiwa na ufahamu wa mazingira hatarishi na vyanzo vya ajali itakuwa msaada mkubwa katika kuepukana na ajali.
“Tunawaomba Watanzania na wageni waweze kubadili fikra na mtazamo ili kuepuka ajali za barabarani na majini,sisi kama wazalendo tupo tayari tunaomba jamii itupokee na ishirikiane nasi kubaini mazingira hatarishi na vyanzo vya ajali kwa pamoja tuweze kupunguza ajali,”ameeleza Ipuli.
Hata hivyo nukuu ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
“Kila sekunde 24 mtu mmoja anakufa kwenye ajali ya barabarani! Ndivyo ulivyoanza ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika maadhimisho ya siku ya kukumbuka waliopoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani Novemba 21,2021,”
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best