May 25, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Elimu ya kijinsia yatolewa Tandale Yemeni

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

SEDEVA ni Taasisi isiyo ya kiserikali inayotumia sanaa kama sehemu ya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu masula ya kijinsia na usawa .

Mradi huo wa vijana network umepata baraka kupitia ngazi ya halmashauri, serikali ya mtaa kwa kuweza kuwafikia watanzania kupitia maonyesho ya sanaa ikiwemo Ngoma , burudani na midahalo mbalimbali.

Akizungumzai katika maeneo ya Tandale Yemeni jijini Dar es salaam Mratibu wa mradi huo Upendo Manase amesema kwamba lengo lake ni kuishirikisha jamii katika masuala mazima ya Afya ya uzazi, malipo ya kazi na kutoa elimu katika usawa wa kijinsia kwa makusudi ya Vijana.

“Mradi huu unatekelezwa nchini Ili kuielimisha wananchi mbinu na changamoto kuhusiana na kufuata Mila na desturi zisizo sahihi za kuwakandamiza akina mama katika ufuatilaji wa majukumu ya kifamilia, Uongozi na mfumo dume,” amesema Manase

Aidha Manase ameeleza kuwa katika project yao wameweza kuwafikia watu mbalimbali kwa kuwapa elimu mbalimbali pamoja na kuendesha midahalo iliyokuwa ikitoa majibu juu ya uelewa wa elimu walioipata.

Hata hivyo Ili jamii iweze kukubali.na kuuelewa masuala mazima ni kuwashirikisha wahusika waweze kutumia Mada mbalimbali zilizo mtambuka ndani ya jinsia na nje Ili kuwezesha mwanamke kutoonekana dhaifu kwa wanaume.

Mratibu huyo amedai kwamba anaziomba Taasisi zingini kuiga mfano wa sevede Ili kuweza kuwafikia waliowengi dhidi ya upatikaji wa elimu dhidi ya uwiano wa kijinsia katika Makundi ya kitanzania na Taifa kwa ujumla